RUFAA YA LEMA YAPIGWA KALENDA.

lema
 Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema( pichani)
 
Na. Vero Ignatus-Arusha
 
Rufaa namba 49/2017 ya mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema imesogezwa mbele kwa ajili ya kutolewa maamuzi mara baada ya upande wa Jamhuri kuiomba mahakama kuu jijini Arusha kuweza kujibizana kwa maandishi juu ya rufaa hiyo ambapo pia jamhuri imesema hawaku pewa nakala ya rufaa hiyo. 

Rufaa hiyo imekuja Mara baada ya lema kufunguliwa kesi ya inayodaiwa kuwa ni ya uchochezi katika mitandao ya kijamii kusambaza kipande cha video kinacho hamasisha maandamo mnamo tarehe 1/9/2016 kuweza kumpinga rais Dkt John pombe magufuli. 

Wakili Shedraki Mfinanga anaemtetea  mbunge Godbless lema  amesema kuwa rufaa hiyo kushindwa kutolewa maamuzi na jaji Dkt Modest Opiyo mahakama kuu ya Arusha ,wameomba wafanye majadiliano kwa njia ya maandishi kwa upande wa jamhuri na upande wa Lema ili waweze kufikia muafaka.

Kwa mujibu wa Jaji Dkt. Modest Opiyo uamuzi wa rufaa hiyo unatarajiwa kutolewa tarehe 27/09/2017 Mara baada ya kusikiza hoja za pande zote. 













 
 








No comments