Kenyatta ashinda uchaguzi wa urais, Raila asusia hafla
88888888888888888888888888888888888888888888888888888888888888888
Tume ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya, IEBC, Ijumaa usiku
ilimtangaza rais Uhuru Kenyatta kuwa mshindi a uchaguzi wa urais
uliofanyika siku ya Jumanne.
Kwa mujibu wa tume hiyo, Kenyatta alipata kura milioni
8,196,313 huku mpinzani wake wa karibu, Raila Odinga akizoa kura
6,793,919.
Akizungumza kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Bomas
of Kenya, mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati alisema uchaguzi wa
mwaka huu ulifanikiwa na kutekelezwa kwa njia ya ustadi.
Muungano wa National Super Alliance (Nasa) ulisusia hafla
hiyo baada ya kuwasilisha malalamiko kwa tume hiyo kwamba uchaguzi huo
uligubikwa na dosari.
Kenyatta alikuwa anawania muhula wa pili baada ya kumshinda
Odinga kwenye uchaguzi wa mwaka wa 2013, ambao mshindi wake aliamriwa na
mahakama ya juu.
Akihutubia waliohudhuria kikao hicho, Kenyatta alimshukuru
mpinzani wake Raila Odinga, na kutoa wito kwake kujiunga naye kwa ujenzi
wa taifa.
“Kama ambavyo nimekuwa nikisema, mashindano ya kisiasa si uadui,” alisema.
Alishukuru tume ya IEBC kwa kile alichokiita “kazi nzuri sana.”
Wakenya 15,073,602 walipiga kura kwenye uchaguzi huo uliokuwa
na ushindani mkubwa amnbapo wagombea kutoka maeneo ya uwakilishi bunge
290 pia waling’ang’ania nyadhifa mbalimbali.
Tangu uchaguzi huo kufanyika, viongozi wa muungano wa NASA,
walianza kutoa malalamiko na kushutumu tume hiyo kwa kile ilichokiita
“kusimamia zoezi lisilokuwa na maana au ukweli woyote.”
Uhuru, mwenye umri wa miaka 56, alifanya kampeni
iliyosisitiza miradi aliyoanzisha tangu kuchukua usukani mnamo mwaka wa
2013. Mgombea wake mwenza nalikuwa ni naibu wake wa rais, William Samoei
Arap Ruto, mwenye umri wa miaka 50.
Wengi wa waangalizi wa kimataifa walikuwa wamesema kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa wazi na wa haki.
Haikujulikana mara moja ni hatua gani Odinga na viongozi wengine wa NASA walinuia kuchukua baada ya tangazo hilo.

No comments