WASTAAFU PSPF MWAKA 2017/18 "KULAMBA" SHILINGI TRILIONI 1.3 ZA MAFAO
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, aliongozana na
Mkurugenzi wa Uendeshaji Bi. Neema Muro na Mkurugenzi wa Mipango na
Uwekezaji Bw. Gabriel Silayo, baada ya kufungwa kwa semina kwa wastaafu
watarajiwa wa wilaya zote za mkoa wa Mwanza iliyofanyika ukumbi wa chuo
cha watumishi wa Benki Kuu ya Tanzania, huko Capri-point jijini Mwanza.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
Katika
hotuba yake aliyotoa Kati wa ufunguzi rasmi wa semina hiyo, Bw. Mayingu
alisema, PSPF inatarajia kulipa wastaafu kiasi cha shilingi Trilioni
1.3 kwa mwaka huu tu wa 2017/18."Kwa mwaka 2017/18 pekee, Mfuko
unatarajia kuwalipa wastaafu 9,552 jumla ya mafao yanayofikia
shilinginTrilioni 1.3.
Kisai
hiki cha Mafao ni kikubwa, hivyo kupitia semina hii Wastaafu watarajiwa
wa PSPF wamejifunza namna ya kupanga maisha yao baada ya kustaafu ikiwa
ni pamoja na fursa za uwekezaji wa mafao yao ili mafao haya yaweze kutoa
mchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi na kuongeza fursa za ajira."
Alisema Bw. Mayingu katika hotuba yake.
Miongozi
mwa mambo waliojifunza wastaafu hao wanaokadiriwa kufika 450, ni pamoja
na uanzoshwaji wa viwanda vidogo vidogo, namna bora ya utunzaji fedha
kwenye taasisi za fedha, (mabenki), lakini pia mbinu mbalimbali za
ujasiriamali.
Kuhusu
mafunzo yaliyotolewa na SIDO, Bw. Mayingu alisema Mfuko ulikutana na
Shirika la Kuhudumia Viwanda vidogo vidogo (SIDO) na kujadiliana namna
ambavyo taasisi hizi mbili zinaweza kushirikiana na kuwafanya wastaafu
wa PSPF wapate ujuzi wa kuwekeza na kuweza kutengeneza ajira kwa
vijana.
"Lengo
likiwa SIDO iwajengee uwezo kitaalamu na kuwapatia vifaa ili wastaafu
wa PSPF waweze kuanzisha viwanda vidogo vidogo na shughuli nyingine za
uzalishaji." Alisema Bw. Mayingu. Alisema wameamua kufanya hivyo kwa
kzuingatia ukweli kuwa, katika kufuatilia wastaafu wa Mfuko wamegundua
kuwa baadhi yao hujiingiza katika biashara mbalimbali ambazo
hawakujiandaa vema na matokeo yake kupoteza mafao yao.
Washiriki wakijadiliana
Mkurugenzi
wa Masoko wa wa Mfuko wa uwekezaji wa pamoja UTT-AMIS, Daudi Mbaga,
akitoa mada ya namna wanachama wa taasisi hiyo wanavyoweza kufaidika kwa
kuwekeza kwenye Mfuko huo.
Mshiriki akizungumza kwenye semina hiyo wakati wa ufungaji wa mafunzo ya siku mbili
Mmoja
wa wastaafu wa PSPF, ambaye kwa sasa ni mteja wa benki ya NMB, akitoa
ushuhuda jinsi alivyofaidika baada ya kuitumia benki hiyo pale
alipostaafu ambapo sasa anaedesha miradi mbalimbali kufuatia mikopo
anayompewa na benki hiyo na kumfanya aishi maisha ya amani.
Mkurugenzi
Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, (kushoto), Mkurugezni wa Uendeshaji,
Bi.Neema Muro, (katikati) na Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji, Bw.
Gabriel Silayo, wakifurahia michango ya mawazo kutoka kwa washiriki wa
semina.
Meneja
wa Mfunzo kutoka Shirika la Kuhudumia Viwanda vidogo vidogo SIDO, Bi.
Beata Minga, (kulia), akiongoza kikao wakati wa kufungwa kwa semina ya
siku mbili ya mafunzo kwa wastaafu watarajiwa
Mshiriki akichangia mawazo yake kwenye semina hiyo
Mkurugenzi
Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, (katkati), akiwa na viongozi wengine wa
Mfuko kutoka kushoto ni Meneja Mipango na Utafiti, Bw.Luseshelo Njeje,
Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bi. Neema Muro, Mkurugenzi wa Mipango na
Uwekezaji, Bw. Gabriel Sulayo, na Meneja wa Pensehini za Wastaafu,
Bw.Mohammed Salim.
Bw. Mayingu, (kushoto), akijadiliana jambo na Bwana
Dominic Haule, Mkurugenzi IMADS, (wakwanza kulia), wengine
wanaosikiliza kutoka kushoto ni Bi. Neema Muro, Bw. Gabriel Silayo,
Bw.Bw.Luseshelo Njeje na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul
Njaidi, baada ya kufungwa kwa semina hiyo
Mgeni
Rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia
Suluhu Hassan, ambaye awali aliifungua rasmis semina hiyo, akiwa katika
picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji,
(watatu kulia waliokaa), Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw.John Mongella,
(watatu kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, (wapili
kulia), na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa PSPF, Bw.Nyakimuro
Muhoji, viongozi wengine na wafanyakazi wa PSPF
Kaimu
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa PSPF, Bw.Nyakimuro Muhoji, (kushoto)
na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa PSPF, Bi. Neema Muro wakiwasili ukumbini
Naibu
waziri wa fedha na mipango, Dkt. Asshatu Kijaji, Kaimu Mwenyekiti wa
Bodi ya Wadhamini ya PSPF, Bw. Nyakimuro Muhoji (katikati) na Mkurugenzi
Mkuu, Bw. dam Mayingu wakiwasili ukumbini.














No comments