RC Ana Mghwira atembelea familia ya Ndesamburo na kutoa Pole.
Baada
ya kutia saini kitabu cha wageni katika ofisi yake mpya leo Alhamisi,
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mgwhira, ameenda kuhani msiba wa
aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema, mkoa huo, marehemu Philemon Ndesamburo.
Mghwira ametoa rambirambi kwa familia ya Ndesamburo, aliyewahi kuwa mbunge wa Moshi Mjini kwa awamu tatu mfululizo.
Mghwira
aliyeteuliwa hivi karibuni na Rais John Magufuli amewasili katika eneo
lake jipya la kazi ikiwa ni siku mbili tu baada ya kuapishwa na Rais,
Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mghwira
anaanza kazi wakati Chama cha ACT-Wazalendo kikimuondoa katika nafasi
yake ya Mwenyekiti wa chama hicho kutokana na matakwa ya katiba ya chama
hicho.
Hata hivyo, Mgwhira ataendelea kuwa mwanachama wa ACT-Wazalendo.

No comments