MRADI WA HIPZ WAANDAA MBIO ZA BASKELI KUKUSANYA FEDHA KWA AJILI YA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA HOSPITALI YA MAKUNDUCHI NA KIVUNGE
Mratibu
wa resi za baskeli (Bike Ride 2017) Dkt. Jon Rees akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu dhamira ya mbio hizo Zanzibar ikiwa ni mara
yake ya tatu.
Mkurugenzi
Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Fadhil Abdalla Mohd akizungumza na
washiriki wa resi za baskeli kabla ya kuanza rasmi zikiwa na lengo la
kuimarisha huduma za afya Hospitali ya Kivunge na Makunduchi.
Picha ya pamoja ya washiriki wa Bike Ride 2017 wakifurahia mbio hizo kabla ya kuanza rasmi.
Washiriki wa Bike Ride 2017 wakijaanda na safari ya kilomita 300 itakayowachukua muda wa siku sita kuzunguka kisiwa cha Unguja.
Washiriki
wa resi za baskeli (Bike Ride 2017) wakikata maeneo ya viwanja vya
Maisra kuendelea na safari yao itakayochukua sita sita.
Picha na Makame Mshenga.
…………………………………………………………………………….
Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar
Mradi
wa Kuimarisha huduma za Afya Zanzibar (HIPZ) unatarajia kukusanya zaidi
ya dola za Marekani 25,000 kwa ajili ya kusaidia huduma za afya katika
Hospitali ya Makunduchi na Kivunge ambazo wanazisaidia.
Fedha
hizo zitapatikana kufuatia kuandaa resi za baiskeli za kilomita 300
(Bike Ride 2017) katika mikoa mitatu ya Unguja yatakayo dumu kwa muda wa
siku sita kuanzia leo.
Akizungumza
na waandishi wa habari Hoteli ya Tembo, Mratibu wa resi hizo Dkt. Jon
Rees kutoka Uingereza amesema jumla ya wapanda baiskeli 25 kutoka Ulaya
na Zanzibar wanashiriki.
Amesema
fedha hizo zitachangwa na makampuni ya ndani na nje ya nchi na
zitatumika kuimarisha huduma za afya hasa afya ya mama na mtoto katika
Hospitali za Kivunge na Makunduchi.
Amesema
Resi hizo ambazo ni mara ya tatu kufanya Zanzibar zilianzia Mji
Mkongwe kuzunguka maeneo mbali mbali ya Mkoa Mjini Magharibi zitapitia
Nungwi, Makunduchi, Kizimkazi na zitrejea Mji Mkongwe.
Dkt. Ress amewataka wananchi wa Zanzibar kuwaunga mkono na kuwatia hamasa wapanda baiskeli hao hasa katika sehemu watakazopita.Akizindua
resi hizo, Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dkt. Fadhil Abdalla Mohd
amesema Mradi wa HIPZ umeleta mafanikio makubwa katika ubunifu wake wa
kutafuta fedha kwa ajili ya huduma za afya kwa kuanzisha mbio hizo.
Amesema
pamoja na kukusanya fedha kwa ajili ya huduma za afya pia mbio hizo ni
sehemu ya kuwashawishi vijana kufanya mazoezi ambayo ni moja ya njia ya
kujikinga na maradhi yasiyoambukiza.
Dkt.
Fadhil amesema wakati serikali ipo katika mpango wa kuzipandisha daraja
Hospitali ya Makunduchi na Kivunge kuwa za Mkoa, fedha hizo zitatumika
kuanzisha majengo mapya na kuimarisha huduma za afya.
No comments