DK. SHEIN ATOA MSAADA KWA WANANCHI WA PEMBA WANAOISHI KWENYE MAZINGIRA MAGUMU, WALIOATHIRIKA NA MAFURIKO
DK. SHEIN ATOA MSAADA KWA WANANCHI WA PEMBA WANAOISHI KWENYE MAZINGIRA MAGUMU, WALIOATHIRIKA NA MAFURIKO
MAGODORO
80 yaliotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi
Zanzibar, dk Ali Mohamed Shein, yakiwa kwenye uwanja wa jengo la Mkuu
wa Mkoa wa kusini Pemba, kabla ya kugawiwa kwa waathirika wa mvua wa
mkoa huo, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
MKUU
wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla, akiwakabidhi wakuu wa
wilaya za Mkoani Hemed Suleiman Abdalla na Mkuu wa wilaya ya Chakechake
Salama Mbarouk Khatib, kila wilaya magodoro 40, yaliotolewa msaada na
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, dk Ali
Mohamed Shein, kwa ajili ya aathirika wa mvua wa wilaya zao, (Picha na
Haji Nassor, Pemba).
MKUU
wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla, akiwakabidhi wakuu wa
wilaya za Mkoani Hemed Suleiman Abdalla na Mkuu wa wilaya ya Chakechake
Salama Mbarouk Khatib, kila wilaya magodoro 40, yaliotolewa msaada na
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, dk Ali
Mohamed Shein, kwa ajili ya aathirika wa mvua wa wilaya zao, (Picha na
Haji Nassor, Pemba).
MKUU
wa wilaya ya Mkoani Hemed Suleiman Abdalla, akitoa neno la shukuran,
mara baada ya kukabidhiwa magodoro 40 na Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba,
Mwanajuma Majid Abdalla, kutoka kwa rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Zanzibar dk Ali Mohamed Shein kwa ajili ya
waathirika wa mvua, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
UNGA
wa ngano polo 112, uliotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Zanzibar, dk Ali Mohamed Shein pmoja na Mchele na
Sukari idadi kama hiyo, kwa ajili ya wananchi wa Pemba, wanaoishi kwenye
mazingira magumu, ambapo chakula hicho ni sadaka, inayotolewa kila
mwezi wa ramadhan na rais wa Zanzibar kwa ajili ya futari, (Picha na
Haji Nassor, Pemba).
MJUMBE
wa kamati ya zaka na sadaka ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi, ndgu Haji Nassib Nyanya, akimkabidhi kwa Mkuu wa Mkoa wa
Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla, mchele, sukari na unga wa ngano,
chakuka chenye thamani ya shilingi milioni 40, ikiwa ni sadaka
iliotolewa na Rais Zanzibar, kwa ajili ya futari ya wnananchi wanaoishi
kwenye mazingira magumu kisiwani Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
MKUU wa Mkoa wa kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla akizungumza kabla
ya kuwakabidhi wakuu wa wilaya ya Mkoani na Chakechake, saruji paketi
150 kila wilaya, zilizotolewa na Rais wa Zanzibar, kwa ajili ya wananchi
waliokumbwa na mafuriko ya mvua ilionyesha hivi karibuni, (Picha na
Haji Nassor, Pemba).
MKUU
wa Mkoa wa Kusini Pemba Mwanajuma Majid Abdalla, akiwakabidhi wakuu wa
wilaya za Mkoani Hemed Suleiman Abdalla, na Mkuu wa wilaya Chakechake,
Salama Mbarouk Khatib, saruji paketi 150 kila wilaya, iliotolewa na Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar dk Ali
Mohamed Shein, kwa ajili ya waathirika wa mvua, (Picha na Haji Nassor,
Pemba).
No comments