UVCCM WATOA TAMKO ARUSHA.
Mbunge wa wanawake Mkoa wa Arusha Catherine Magige akiwa ameongozana na mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Arusha Lengai Ole Sabaya pamoja na katibu hamasa wa mkoa, wakiangalia uharibifu uliotokea kutokana na kuungua moto Shule ya Sekondari ya Mlangarini iliyopo manispaa ya Arusha vijijini ,Halmashauri ya Arumeru.
Habari na Vero Ignatus Arusha
Kutokana kukithiri kwa uchomaji.wa shule katika Mkoa wa Arusha ,Umoja wa vijana wameitaka serikali mkoani hapo,kubaini ni nani anayehusika na ninini chanzo cha tatizo hilo,ambapo matukio hayo yamekuwa yakifanana kwa.kuchomwa kwa mabweni ya wavulana nyakati za usiku,amabapo wanafunzi wanakua katika masomo ya jioni ambapo hali hiyo imewaweka katika sintofafamu ukizingatia wengne wanajiandaa na mitihani ua ktaifa ya kidato cha pili na cha nne na ile ya mwisho wa mwaka.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Arusha alipotembelea shuleni hapo kuangalia uharibifu uliosababishwa na moto huo ambapoamesema wamechoshwa na mayukio hayo kusikia na kutokupatiwa ufumbuzi wa tatizo hilo.
Amesema kuwa ili kuihakikisha mtandao huo unakomeshwa na kutokomezwa kwani imekuwa likiingizia serikali.hasara pamoja na wadau mbalimbali wanaochangia maendeleo.ya shule,pia imekuwa ikiwatia hofu wanafunzi kuendelea masomo yao na mara nyingi wamekuwa wakiathirika kisaikolojia.
Kwa upande wake Mbunge wa wanawake mkoa wa Arusha Catherine Magige,amesema kuwa hawapo tayari kuchangia wanafunzi kutokana na mioto hiyo ya mara kwa mara hadi pale watakapopewa taarifa za mtu ambaye anahusika na matukio hayo,ambapo tabia hiyo ikiendelea italqeta maafa kwa watoto wetu.
Magige amemuomba waziri mkuu Kassimu Majaliwa kuingilia kati swala.hili hususani mkoa wa Arushakwani kuendelea kuchangia haitamaliza tatizokwani tutachangia hadi lini?alihoji Mbunge huyo.
Kwa upande wake Kamanda wa Uvccm Mkoa wa Arusha Philemon Olais Mollel ameitaka kamati ya ulinzi na usalama mkoani hapa kitoa majibu ya uunguzwaji wa shule haswa mabweni yawavulanakatika shule hizo tano ndani ya mwezi mmoja ,Sambamba na hilo kamanda huyo wa vijana ameahidi shilingi milioni moja kwa atakayemfahamu mtu anayesababisha matukio.hayo ya mara kwa mara.
.
Mbunge wa wanawake mkoa wa Arusha Catherine Magige akiwa anasaini kitabu cha wageni katika ofisi ya shule ya Mlingarini alipotembelea kuwaona baada ya bweni la wavulana kuungua moto.
Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Mlingarini Mathius Manga
Mkuu wa shule msaidizi Mohamed Billal akiwa nje ya ofisi ya shule hiyo baada ya kuwapokea wageni waliotembelea shuleni hapo baada ya bweni la wavulana kuungua.
Muonekano wa bweni la wavulana katika shule ya Sekondari Mlingarini,baadhi ya vifaa vya wanafunzi yakiwemo madaftari,sare za shule.na masanduku ya kuhifadhia vifaa vyao vikiwa vimeharibiwa vibaya na moto huku madafutari ya kutunzia kumbukumbu yakiwa yameungua pia.
Bweni lililoungua kama linavyoonekana kwa ndani.
Pamoja na shule hiyo ya Mlingarini kupata shoruba ya kungua bado wanagunzi wanaendelea na masomo kama kawaida kama unavyoona picha wanafunzi wakiwa wametoka darasani tayari.kwa kuelekea majumbani.na wengine kubaki shuleni hapo maana shule hiyo ina wanafumzi wa kutwa na wanaolala shuleni hapo.
No comments