Kingunge awashauri viongozi wastaafu

Mwanasiasa mkongwe nchini KINGUNGE NGOMBALE MWIRU amewashauri
marais na Mawaziri wakuu wastaafu nchini kuingilia kati mvutano kati ya
Chama cha Demokrasia na Maendeleo -CHADEMA na serikali wa kutaka
kufanya mandamano na mikutano nchi nzima bila kibali cha kufanya hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake jijini DSM KINGUNGE
amesema viongozi hao wana nafasi kubwa ya kutafuta suluhu ya mgogoro huo.
Tayari viongozi mbalimbali wa dini na serikali wameshauri kuwepo kwa
maridhiano kati ya serikali na CHADEMA.

Hapo jana Msajili wa Vyama vya siasa nchini jaji FRANCIS MUTUNGI
alitangaza kuwepo kwa kikao tarehe 26 mwezi huu na kisha Baraza la Vyama
vya Siasa nchini tarehe 29 na 30 mwezi huu kwa lengo la kujadili hali ya kisiasa
nchini
CHADEMA imepanga kufanya mikutano na maandamano nchi nzima Septemba
Mosi mwaka huu.

Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi mkoani MBEYA limewahakikishia wananchi
wa mkoa huo amani na utulivu katika kipindi cha kuelekea maandamano
yaliyoandaliwa na vyama vya siasa Septemba Mosi mwaka huu.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya BUTUSYO MWAMBELO,
ametoa kauli hiyo baada ya kuhitimisha mazoezi ya kawaida ya Jeshi hilo
ambayo yamefanyika kuzunguka viunga mbalimbali vya Miji ya Mbeya na
Mbalizi.

No comments