Update: Majambazi Kadhaa Yauawa Katika Mapigano na Jeshi la Polisi huko Mkuranga

Majambazi ambao idadi yao haijajulikana wanadaiwa kuuwawa katika mapigano
hayo kati yao na polisi huko Vikindu, wilaya ya Mkuranga leo.

Milio ya risasi na mabomu vilisikika kuanzia saa saba usiku katika eneo hilo
ambalo majambazi hayo walikuwa wamejificha.

Habari zilizotufikia hivi punde, zinaeleza kuwa Polisi wameweka kizuizi cha
barabara eneo la Kongowe, wilayani Mkuranga ambapo magari yote yanayotoka
na kuingia Dar yanapekuliwa.



No comments