Waliofariki Italia waongezeka, manusura watafutwa


Idadi ya watu waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi katikati mwa Italia
mapema Jumatano imefika 247 huku manusura wakiendelea kutafutwa.
Maafisa wa uokoaji wanaendelea na juhudi za kutafuta manusura na miili
kwenye vifusi.
Tetemeko hilo la nguvu ya 6.2 katika vipimo vya Richter liliharibu vibaya miji ya
Amatrice, Accumoli na Pescara del Tronto ambapo watu wengi walifariki.
Maafisa wa uokoaji waliendelea na juhudi za kuwatafuta manusura usiku, lakini
wakati mmoja walitatizwa na mitetemeko mingine iliyotokea na kutikisa
majumba yaliyosalia yakiwa bado wima.
Eneo lililokumbwa na tetemeko hilo ni milimani katika majimbo ya Umbria, Lazio
na Marche.
Kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa karibu na Norcia, kilomita 170 kaskazini
magharibi mwa mji mkuu Roma.
Mahema yamewekwa kuwasaidia watu walioachwa bila makao.

No comments