Waasi nchini Colombia wasaini mkataba wa amani
Serikali ya Colombia na kundi la waasi la Farc wamesaini mkataba wa amani
kusitisha mgogoro uliopo zaidi ya miongo mitano.
Pande zote mbili zimekubaliana kusaidia jamii, kuwapa haki zao waathirika wa
mgogoro huo na kuleta amani.
Tamko la pamoja limesomwa katika sherehe zilizofanyika mji mkuu wa Cuba
huko Havana,ambapo makubaliano hayo ya amani yalianzishwa karibu mika 4
iliyopita.
Mgogoro huo umesababisha vifo vya watu zaidi ya laki mbili na kuaawacha
zaidi ya milioni bila ya makazi huko colombia.
Muda wa makubaliano wa mkataba huo bado unahitajika kuwekwa na
wananchi wa Colombia kupitia kura ya pamoja itakayofanyika mwezi oktoba.
No comments