UCHELEWESHAJI WA KESI ZA WATOTO WAKWAMISHA HAKI ZA WATOTO
Vero Ignatus Arusha
Ucheleweshaji wa kesi za watoto walioko katika mahabusu za watoto umetajwa kuwa chanzo cha kukwamisha haki za watoto na kuwasababisha mlundikano katika mahabusu hizo hivyo kukosa haki ya elimu na malezi ya familia.
Baadhi ya watoto Bertha Jukaeli na Rose Wiliam waliopata msaada wa kisheria kutoka shirika lisilokua la kiserikali la Valonteer Tanzania Abroad ,wamesema kuwa licha ya kupata mawakili waliowasaidia bado kuna idadi ya watoto wanaokosa mawakili hivyo kushinda kujiwakilisha vyema mahakamani na kukosa haki zao.
Wameiomba serikali na Mashirika binafsi na Mawakili wa kujitegemea kuhakikisha kuwa watoto wanapata mawakili ili waweze kupata haki zao na kurejea katika jamii ili kujenga jamii bora na yenye ustawi mzuri.
Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Arusha Musa amesema kuwa miundombinu iliyoko katika mahabusu za watoto si rafiki kwa maana ya kukosekana kwa madarasa hivyo watoto wanapokaa muda mrefu wanapoteza haki zao za elimu ,pia ameiomba serikali ifanye maboresho katika mahabusu hizo.......
Kwa upande wake Mmmoja wa Wageni wanaojitolea kutoka nchini Ufaransa Ezis John anasema kuwa kuna uwazi mkubwa kutoka kwenye sheria na uhalisia wajamii bado haki za binadamu ni changamoto hususan kinamama na watoto pia wanaume wanapaswa kuhusishwa.
No comments