27 WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI ARUSHA

Kutokana na majanga ya  kuungua moto kwa shule za sekondari katika wa Mkoni Arusha  
 jeshi la polisi  linawashikilia washukiwa wapatao 27 wakiwemo Wanafunzi, Walimu pamoja na Rai wa
kawaida wakihushishwa na matukio hayo ya  uchomaji wa  moto shule 6 huku jeshi hilo likiendelea
kusaka mfadhili wa mtandao huo wa kihalifu.

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo  amezungumza na waandishi wa habari ofisini kwake  na kusema  kuwa tukio jingine limetokea majira ya saa saba usiku na taarifa za kiintelejensia zinaeleza kuwa kuna kundi la watu linalofadhili watu wanaofanya uhalifu huo.

Shule binafsi ya Sekondari ya Winning Spirit ,iliyopo katika kata ya Kiranyi imeteketea kwa moto ikiwa ni muendelezo wa matukio mbali mbali ya uchomaji
wa shule yanayofanywa na watu wasiofahamika.

Aidha  Kamanda  Charles Mkumbo amesema kuwa matukio hayo yalianza kujitokeza
kuanzia Julai 31 mwaka huu ambapo shule mbali mbali toka wilaya za Munduli,
Karatu, Longido, Arumeru na Arusha Dc zimeathiriwa na matukio hayo.Jeshi la polisi linafanya uchunguzi wa kina kuubaini mtandao huo na kuchukua hatua za kisheria.










No comments