Diwani mbaroni kwa uchochezi.
Masaa machache baada ya Kamanda mkuu wa polisi Charles Mkumbo kutangaza kuwepo kwa kikundi kinachotaka kufanya vurugu mkoani hapo ,polisi wamemshikilia diwani wa chadema kata ya Sombetini Ally Bananga kwa tuhuma za kufanya uchochezi
Diwani huyo alishikiliwa juzi na polisi baada ya video zake kusambaa kwenye mitandao ya kijamii zinazomuonesha akihamasisha maandamano ya UKUTA
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo, amekiri kukamatwa kwa Diwani huyo na kusema kuwa diwani huyo anatuhumiwa kwa kosa la kufanya uchochezi hivyo atapandishwa kizimbani baada ya uchunguzi kukamilika
Pia alisema Polisi walienda kufanya uchunguzi nyumbani kwa diwani huyo na hana taarifa kilichopatikana ila upelelezi bado unaendelea kufanyika na utakapomalizika watapeleka jalada la kesi kwa mwanasheria wa serikali
Upande wa wawakili anayesimamia kesi hiyo ya Mwanasheria na Diwani , James Lyatu ameliambia amesema kuwa mpaka sasa diwani huyo anashikiliwa na jeshi la polisi kwaajili ya mahojino hivyo wanasubiri muda wowote kwenda mahakamani
Pia alisema baada ya polisi kwenda nyumbani kwa diwani huyo wameweza kuchukua Fulana ya diwani huyo iliyokuwa imeandikwa "UKUTA "
"Diwani yuko salama nimemuona ,tunasubiri upelelezi utakapokamilika wamfikishe mahakamani,"alisema James
Licha ya kuwepo kwa taarifa za kutafutwa kwa Mwenyekiti wa chadema mkoa wa Arusha ,Amani Golungwa na Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ,mwenyekiti huyo nae amesema amesikia taarifa hizo japo yeye hazijui ukweli wake
Pia alisema kukamatwa kwa kiongozi huyo haiwezi kurudisha nyuma mipango yao ya kufanya maandamano kupinga udikteta wa rais Magufuli hivyo kama chama wako mbele kuendelea na mipango yao
Alisema serikali ijiandae kwa matukio ya mfululizo kuendea mosi septemba na kwamba hawataacha walichodhamiria mpaka pale serikali itakapokuwa tayari kusikiliza madai yao
"UKUTA si tu kwa viongozi hata wananchi wanapenda mabadiliko na wanaunga mkono maandamano hayo ,hivyo hta wakikamata viongozi wote ,bado UKUTA iko paleplae ,"alisema Amani
Pia alisema kwa kanda ya kaskazini wamejianda vyema kuendea siku hiyo ya septemba 1 hivyo hawana hofu na lolote.

No comments