CWT Arusha yahofia uhakiki wanafunzi hewa


Rais wa chama cha walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba,


ARUSHA.

Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Arusha,
kimetaka uhakiki wa wanafunzi hewa jijini hapa kuanza upya
kwa madai ya uwapo wa uamuzi wa chuki dhidi ya wakuu wa
shule.

Ameyasema hayo ofisini kwake  Makamu Mwenyekiti wa CWT
Mkoa wa Arusha, Andrew Ngazu ,ya kwamba chama hicho kinamtaka
mkurugenzi wa jiji kurudia uhakiki wa wanafunzi kwa sababu uamuzi
uliotolewa ulikuwa wa binafsi na haukufuata utaratibu
maalumu.

“Tunamuunga mkono Rais Johh Magufuli kuhakiki shule zenye
wanafunzi hewa, ila tunapinga kwa nguvu zote uhakiki
uliofanyika Arusha,” alisema Ngazu na kuongeza: “Tunaamini
umefanywa na maofisa wa elimu kwa chuki dhidi ya walimu
wa shule, hali iliyosababisha kuonewa kwa baadhi ya walimu
huku shule zenye wanafunzi hewa zikiachwa.”

Makamu Katibu wa CWT, Nurueli Kavishe alisema mpaka sasa wana ushahidi
unaojitosheleza kuwa mwajiri wao ambaye ni mkurugezi wa
jiji hakutumia takwimu zilizopo.

Katibu wa CWT Wilaya ya Arumeru, Joyce Kizaji aliwataka
wakurugenzi kuacha kuwatisha walimu kuhusu Mwenge kwani
siyo lazima.







No comments