Wahandisi 347 wafutiwa usajili
Dar-es-salaam
Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB) imewafutia
usajili wahandisi 347 kwa makosa mbalimbali ya kimaadili
katika taaluma hiyo katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.
Msajili wa ERB, Injinia Steven Mlote amesema jana kuwa baadhi
ya makosa hayo ni kusimamia kazi ambazo zilikuwa chini ya
kiwango.
Injinia Mlote amesema hayo wakati akitangaza siku ya wahandisi
ambayo itafanyika kesho, Septemba Mosi na Rais John Magufuli
atakuwa mgeni rasmi ambako atashuhudia wahandisi 200 wakila
kiapo cha utii.
“Watakula kiapo mbele ya Rais Magufuli ili kuhakikisha
wanawajibika vyema kwa kufuata maadili kwenye taaluma yao,”
amesema.

No comments