MIAKA 50 YA KAMPUNI YA BIMA YA BRITAM.

Habari na Vero Ignatus Arusha.

Hatimaye Kampuni ya Bima ya Britam imeadhimisha miaka 50 ya kutoa huduma
za bima nchini Tanzania huku ikiongoza katika utoaji wa huduma
bora za bima za magari,nyumba ,mali pamoja na afya.

Sherehe za Maadhimisho hayo zimefanyika katika Hotel ya Mount
Meru iliyoko jijini Arusha na kuudhuriwa na Viongozi wa kiserikali
pamoja na Wadau wa Bima.

Afisa Mkuu wa Kampuni hiyo nchini Tanzania Stephen Lokonyo
amesema kuwa kampuni hiyo imejipanga vizuri kuwahudumia
watanzania na kuwafikia watu wengi zaidi ili waweze kunufaika na
huduma za bima .

Aliongeza kuwa wao kama kampuni ya bima ya Britam wamejipanga
kuwasaidia wananchi mbalimbali wakiwemo wa juu pamoja na
wachini kwakuanzisha bima za aina mbalimbali ikiwemo ya mali zao
kama nyumba ,bima za afya pamoja bima ya kilimo kwa ajili ya
wakulima pamoja na wafugaji.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mrisho Gambo aliwataka mashirika ya
bima kuwafikiria pia madereva bodaboda kwa kuwaanzishia bima za
afya pamoja na bima za vyombo vyao ili pale wanapopata matatizo
kama ya kuunguliwa na piki piki zao pamoja na kupata ajali waweze
kusaidika kwa uraisi matibabu na kufidiwa pindi wanapopata ajali.

Alisema kuwa kumekuwa na pikipiki nyingi sana hivyo iwapo
wataanzisha bima kwa ajili ya pikipiki wataweza kuwasaidia sana
vijana pia wataweza kupata wateja wengi waotumia vyombo hivi.
Aidha mkuu huyo wa wilaya alihiasa kampuni ya bima ya Britam
pamoja na kampuni zingine za bima kujikita zaidi kwa watu wenye
kipato cha chini.
Meneja BRITAM Tanzania tawi la Arusha Bi. Loisi Yatera
akiwatambulisha baadhi ya watendaji wa Kampuni hiyo mbele ya
wageni waliohudhuria katika hafla hiyoKatikati ni Mgeni rasmi mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Mh.Mrisho
Gambo ambaye alikuwa akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Mh.Daudi Ntibenda, akipongezana na Mkurugenzi wa Masoko BRITAM
Kenya huku miale ya baruti ikihanikiza ishara ya uzinduzi wa
shughuli zitakazokuwa zikifanywa na BRITAM katika jiji la Arusha
wakati wa hafla hiyo katika hoteli ya Mount Meru.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Mh.Mrisho Gambo akihutubia
wageni katika hafla hiyo
Kulia ni Mgeni rasmi mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Mh.Mrisho
Gambo ambaye alikuwa akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Mh.Daudi Ntibenda, akifungua pazia ishara ya uzinduzi wa shughuli
zitakazokuwa zikifanywa na BRITAM katika jiji la Arusha wakati wa
hafla hiyo katika hoteli ya Mount Meru
Mkurugenzi mtendaji BRITAM Tanzania Bw.Stephen Lokonyo akitoa
historia ya utendaji wa kampuni kuhusu kampuni yao wakati wa
hafla hiyo katika hoteli ya Mount Meru (picha zote na Dickson
Mulashani)
Mkurugenzi mtendaji BRITAM Tanzania Bw.Stephen Lokonyo akitoa
historia ya utendaji wa kampuni kuhusu kampuni yao wakati wa
hafla hiyo katika hoteli ya Mount Meru (picha zote na Dickson
Mulashani)
Kutoka kulia ni Afisa Mkuu wa Uendeshaji BRITAM Bw.Sodson
Manatsa akiwa na Meneja Masoko BRITAM Tanzania Bw.Godfrey
Mzee wakifuatilia kwa makini hafla hiyo.

Meza kuu walipokaa wageni rasmi katika hafla hiyo.
Meneja BRITAM Tanzania tawi la Arusha Bi. Loisi Yatera.
Kutoka kushoto ni Mbunge wa zamani wa jimbo la Arusha Mjini
Mh.Felix Mrema, katikati ni Mkurugenzi wa Masoko BRITAM Kenya
na mwisho ni Mkurugenzi BRITAM Kenya Bw.Stephen Wandera
MKutoka kushoto ni Mbunge wa zamani wa jimbo la Arusha Mjini
Mh.Felix Mrema, katikati ni Mkurugenzi wa Masoko BRITAM Kenya
na mwisho ni Mkurugenzi BRITAM Kenya Bw.Stephen Wanderabunge wa Atusha Godbless Lema akiwa na Mkewe katika hiyo iliyoandaliwa na kampuni ya Britam katika hotel ya Mount meru

Mkurugenzi wa Britam kutoka Nchini Kenya akimsikiliza kwa.makini mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Arusha Mrisho Gambo.


















No comments