ASKARI POLISI WATATU WAUWAWA JANA USIKU HUKO MBAGALA MMBANDE JIJINI DAR ES SALAAM
Taarifa iliyotufikia jana usiku inaeleza kuwa, kuna tukio la kuuwawa
kwa Askari Polisi, lililotokea huko Mbagala jijini Dar.
Inadaiwa kuwa askari hao walikuwa wakibadilishana lindo katika
Benki ya CRDB tawi la Mbagala Mmbande na mara wakaibuka watu
wanaodhaniwa kuwa ni Majambazi na kuanza kuwashambulia kwa
risasi na baada ya shambulizi wanadaiwa kuondoka na pikipiki
wakielekea maeneo ya Mvuti.
ASKARI WALIOFARIKI ni
E5761 CPL YAHAYA
F4660 CPL HATIBU NA
G9544 PC TTITO.
Inasemekana kuwa tukio hilo limetokea mnamo saa 1: 30 ni katika
tukio la UVAMIZI WA BANK CRDB MBANDE na inadaiwa kuwa
wahalifu hao waliondoka na silaha moja aina ya SMG.
Tukio hili limetokea wakati askari wakibadilishana lindo. Mmoja
aliyefariki alikuwa anaingia, mmoja alikuwa anatoka na mwingine
alikuwa dereva.
Inadaiwa kuwa majambazi hayo hayakuingia ndani ya benki.
Gari la Polisi (Leyland Ashok) limeharibiwa kwa risasi.
Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Simon
Sirro amethibitisha na kusema: "Ni kweli kumetokea tukio la uvamizi
hapa mbagala lakini kwa taarifa kamili ntazitoa leo kwakuwa
bado alikuwa eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi zaidi".

No comments