Jeshi La Polisi Lahusisha Mauaji ya Polisi Wanne na Sakata la Oparesheni UKUTA.........Lapiga Marufuku Mikutano yote ya Ndani ya Vyama vya Siasa
watu wanaodhaniwa ni majambazi kuvamia benki ya CRDB na kuwaua askari
hao kwa kutumia silaha za moto jeshi la Polisi limetangaza kiama na kuwataka
wahusika wote kujisalimisha.
Katika hatua nyingine jeshi la polisi limehusisha tukio hilo na Umoja wa Kupinga
Udikteta Tanzania (UKUTA) kufuatia matamko ya baadhi ya viongozi wa kisiasa
ambao wamesikika katika majukwaa ya kisiasa wakihamasisha wafuasi wao
wawashambulie askari wa Jeshi la Polisi.
Kauli hiyo imetolewa na Kamishna Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi
nchini, Nsato Marijan Mssanzya (CP), wakati akizungumza waandishi wa habari
Dar es Salaam leo mchana ambapo pia alikiri kuwa mazoezi yanayofanywa na
polisi yamelenga kukabiliana na Ukuta.
Akizungumza kwa hisia CP Mssanzya pia amepiga marufuku mikutano ya
ndani yenye viashiria vya uchochezi na hata ikifanyika kwenye majukwaa
watamshusha muhusika na kumfikisha kwenye mkono wa sheria.
Amesema Jeshi hilo limebaini kwamba mikutano hiyo imekuwa ikitumika
kuchochea wananchi na kuwahamasisha kuvunja sheria za nchi na kufanya
mapambano na jeshi la polisi
"Kwasababu hiyo basi,kwa hali ya kutumia mikutano ya ndani kuchochea watu
kuvunja sheria na kupambana na askari, hivyo basi kuanzia sasa jeshi la polisi
nchini linapiga marufuku mikutano yote ya ndani" amesema.
Aidha CP Mssanzya aliwataja askari waliouawa katika tukio hilo wakati
wakibadilishana lindo kuwa ni E.5761 CPL Yahya, F.4660 CPL Hatibu, G 9524
PC Tito na G 9996 PC Gastoni na raia wawili waliojeruhiwa aliowataja kuwa Ali
Chiponda na Azizi Yahya wote wakiwa wakazi wa Mbande.
"Katika tukio hilo majambazi ambao idadi yao haikufahamika walifanikiwa
kupora silaha mbili aina ya MSG na lisasi 60 na hakuna pesa wala mali ya
benki hiyo kuibiwa au kuharibiwa, ni dhahiri kuwa waharifu hao walikuwa na
kusudio moja tu la kuwashambiulia askari polisi, " alisema.
Alisema katika hali ya kushangaza baada ya tukio hilo kuna baadhi ya watu
waliandika mitandaoni kubeza na kukeji mazoezi ya kawaida ya jeshi la polisi
na wengine waliandika ujembe wa kushabikia tukio hilo la kuuawa kwa askari
polisi huku wengine wakidiriki kuandika ujumbe unaosema endapo watapigwa
na polisi Septemba1 mwaka huu basi viongozi wa jeshi hilo wawaondoe askari
wanaoishi uraiani na kuwarudisha kambini.
Aliongeza kuwa jeshi la polisi limejipanga vyema kukabiliana na matukio yote ya
uvunjifu wa amani nchini.

No comments