TFDA :Jukumu la kutunza afya yako ni wewe mwenyewe


Meneja wa TFDA Kanda yaKaskazini Damas Matiko akiwa na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Bendel Memorial Moshi Kilimanjaro.walipotembelea banda hilo la Mamlaka ya chakula na dawa katika viwanja vya Taso nanenane Njiro.


Habari na Vero Ignatus Arusha.

Wito umetolewa na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA watoe ushirikiano wanapowakamata wahalifu   na wanapochukua hatua ,watoe taarifa kwa mamlaka hiyo kwa njia ya simu pale wanapobaini kuwa wanaotengeneza bidhaa bandia mtaani kwao.

Hayo yamesemwa na Meneja wa TFDA kanda ya kaskazini Damas Matiko Nyang'anyi katika maonyesho ya wakulima na wafugaji katika viwanja vya Taso nanenane Themi Njiro ambapo amesema kuwa wafanyabiashara wa maduka ya jumla na rejareja pamoja na supermarket zote wasipokee bidhaa kutoka kwa.wajasiriamali wadogo ambao bidhaa zao hazijasajiliwa na TFDA ,maana hawatambui ubora na usalama wake,bidhaa hizo zikibainika zitachukuliwa nakwenda kuteketezwa.

Hayo ni sambamba na waingizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi ambazo ni.chakula,vipodozi na madawa pamoja na vifaa tiba wanakumbushwa kufuata utaratibu wa kuingiza bidhaa ikiwemo kuomba kibali kutoka mamlaka ya chakula na dawa ,wanatakiwa watambue kuwa TFDA ina wakaguzi mipaka yote 32 ya Tanzania bara hivyo wasijidanganye kuwa wanaweza kukwepa chochote.

Aidha Matiko amesema kuwa wale wote watskao ingiza bidhaa sokoni.zisizosajiliwa na Tfda,      zitakamatwa   zote nakutolewa sokoni,kwa mujibu wa sheria ya chakula na dawa na vipodozi  yamwaka 2003 ambapo inasimamiwa na Mamlaka ya chakula.na dawa TFDA.
Ameongeza.kiwa watu wote wanaoinhiza bidhaa zisizokuwa na ubora au bandia.

"Mlinzi wa afya ya mwananchi ni mwananchi mwenyewe unaponunua bidhaa ni vyema ukaangalia tarehe y a mwisho wa matumizi ili kubaini muda wa matumizi kama upo sahihi au la ,ukibaini muda wake wa matumizi umeisha wu umefutwa toa taarifa TFDA kwa namba ya simu ifuatayo 0752063213.Toa taarifa kama unamashaka na bidhaa ,kama upo mkoa wa Arusha tumia hiyo namba na kama upo nje ya mkoa wa Arusha toa taarifa ofisi yamganga mkuu wa wilaya iliyopo maana wanafanya kazi kwa niaba ya TFDA ,bidhaa katika maeneo hayo alisema Matiko."

Wazalishaji wadogowadogo haswa wasindikaji kina mama.ni.kosa kuzalisha bidhaa na kuingiza sokoni.bilw kusajiliwa na TFDA ,bidhaa hiyo itaondolewa sokoni mara moja n akuteketezwa.


Emmanuel Masunga Mkaguzi wa Dawa Kanda ya Kaskazini akiwa naonyesha sabuni ambayo imepigwa marufuku inamadhara kwa watumiaji ,inatumiwa na wakinadada wengi ambayo inadaiwa ya kurudisha ubikra ambapo inakwenda kusababisha madhara.
Abdallah Mkaza Mkaguzi wa Chakula Kanda ya Kaskazini akionyesha maziwa ambayo yamengizwa sokoni bila usajili wa TFDA.
Baadhi ya vipodozi,Sabuni ya kurudisha ubikira kwa wanawake ambavyo vimepigwa marufuku ma Mamlaka ya chakula na dawa TFDA kama vinavyoonekana katika picha,haviruhusiwi kwa matumizi ya kibinadamu, haviruhusiwi kununuliwa wala kuuzwa maana vina madhara kwa binadamu.

No comments