Diwani wa Chadema afikishwa Mahakamani
Vero Ignatus Arusha
Diwani wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Kata ya Sombetini,Ally Bananga(40),amepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kuhamasisha uchochezi
Akisomewa shauri hilo mbele ya Hakimu Mfawidhi Augustino Rwezire, mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Arusha, diwani huyo anakabiliwa na shitaka la kuhamasisha wananchi kufanya maandamanao yasiyo halali, Septemba mosi mwaka
Diwani huyo alifikishwa mahakamani hapo leo mbele ya Hakimu Mfawidhi,Agustino Rwizile,ambapo Wakili wa Serikali Charles Kagirwa,alidai kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Agosti 13 mwaka huu,wilayani Karatu mkoa wa Arusha.
Pia alisema kuwa siku ya tukio Bananga akiwahutubia wananchi katika mkutano wa wazi uliofanyika eneo la Hosteli ya Karatu, aliwahamasisha wananchi hao washiriki katika kusanyiko lisilo halali ya tarehe 1 septemba
Wakili huyo aliiomba mahakama hiyo kuahirisha kesi hiyo kutokana na upelelezi wake kutokukamilika na kudai kuwa dhamana iko wazi kwa mshitakiwa.
Mawakili wa utetezi John Mallya Wakili James Lyatuu, wameiomba mahakama hiyo kumpa Bananga masharti nafuu ya dhamana kwani ni diwani na anaweza kujidhamini mwenyewe
Hakimu Rwizile alikubaliana na ombi hilo na kumtaka Diwani huyo kujidhamini mwenyewe kwa dhamana ya shilingi milioni 5 na kuahirisha kesi hiyo hadi Septemba 22 mwaka huu ambapo kesi hiyo itatajwa tena.
Nae, Mbunge wa Arusha Mjini,Godbless Lema amesema maandamano ya Septemba Mosi yapo palepale na wamejianda kupambana na polisi
Diwani huyo alitiwa kizuizini kwa siku tatu huku nyumbani kwakwe kukutwa na fulana moja iliyoandikwa UKUTA

No comments