SIMBACHAWENE:TAFITI ZOTE NA GUNDUZI LAZIMA ZIPELEKWE KWA WANANCHI.

Mkuu Mkoa wa Arusha Daud Filex Ntibenda akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadick wakiwa wanamtunza mmoja wa waimbaji wa ngoma ya kipemba katika viwanja vya Taso Themi Njiro (hao vijana ni wa JKT  Oljoro).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi George Simbachawene akiwa anazungumza na wananchi wa katika viwanja vya Taso Themi Njiro katika kilele cha maonyesho ya nanenane Jijini Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadick akiwa anazungumza na wananchi katika  kilele chamaonyesho  ya sikukuu ya wakulima na wafugaji katika viwanja vya Taso Themi  Njiro  Jijini Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daud Filex Ntibenda akiwa anazungumza na wakilima na wafugaji pamoja na washiriki wengine wa maonyesho ya nanenane katika viwanja vya Taso Themi Njiro ambapo siki hiyo ilikiwa kilele cha maonyesho hayo.

Habari na Vero Ignatus Arusha.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi George Simbachawene ,amesema kuwa tafiti nyingi za kilimo na idara za umwagiliaji sekta hizo zimewekwa kwa ustadi mkubwa pia tafiti hizo zimefanywa kwa gharama kubwa,hivyo tafiti hizo zisipopelekwa kwa wananchi wakaanza kuzitumia itakuwa ni kazi bure.

Waziri ameyasema hayo katika kilelecha sikukuuu ya manyesho ya kilimo na mifugo ya nanenane Jijini Arusha ,katika viwanja vyaTaso nanenane Themi Njiro ,ambapo alikuwa mgeni rasmi ,ambapo ametoa rai kwa halmashauri zote katika Mikoa hiyo mitatu kujenga mpango mahususi kila baada ya maonyesho ,waangalie tafiti hizo ugunduzi nyingi zinafikishwa kwa wananchi. 

Amezitaka mamlaka zote nchini  serikali za mitaa wachukue jukumu hilo kuwa ni la muhimu ,wazipeleke kwawananchi, huku akiwataka maafisa kilimo kuendeleza shamba darasa kwa wananchi hupo walipo wakishirikiana na mdiwani katika kata zao maana wao ni rahisi kuwafikia wananchi huko walipo ni rahisi wao kufahamu changamoto ambazo wananchi wanazozipitia katika maeneo yao.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadick amesema kuwa hakuna eneo  linaloweza kutatua shida kubwa ya chakula,zaidi ya kilimo maana hutoapia ajira kwa wananchi,kwenye viwanda na sehemu nyingine mbalimbali, hivyo ni lazima sekta hii itiliwe mkazo zaidi.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Kilimanjaro amezitaja changamoto wanazokitana nazo wajasiriamali wadogowadogo haswa wakina mama wasindikaji, ni ucheleweshaji wa Mamlaka ya Chakula na dawa TFDA kusajili bidhaa zao pamoja na shirika la viwango TBS hivyo inawafanya wajasiriamali hao kutokufanya kazi zao kwa wepesi zaidi, ukilinganisha na lauli mbiu yamaonyesho ya mwaka huu inayosema Kilimo,Mifugo na Uvuvi ni nguzo ya maeneleo:Vijana shiriki Kikamilifu" Hapa kazi tu"

Sambamba na hayo amesema kuwa zana za kilimo zimekiwa ghali sana kiasi chakwamba mkulima mdogo hawezi kuhilili ,hivyo amewataka wafanyabiashara wabnaoagiza zana hizo nje ya nchi wathibitiwe,wasijipangie bei kiholela,ili watu wa hali ya chini waweze kuhimili,amewataka wadau wa pembejeo za kilimo waende kuwaelimisha wakulima ili waweze kuepukana na kilimo cha mkono,wafuate masharti ya kulima mazao kufuatia kanda za kilimo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daud Filex Ntibenda amesema kuwa mwakani 2017 lazima maonyesho yabadilike,huku akizitaka halmashauri zilizopo katika mikoa yote mitatu kuwa makini,waandae mabanda mapema na yawe ya kisasa,kuwepo na ukumbi wa kisasa wa Taso.
Wa kwanza kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitwega,kulia kwake akifuatiwa na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadic,anayemfuata kulia kwake ni Mwenyekiti wa Taso kanda yaKaskazini Athar Kitonga Shayo,Akifuatiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya raisi Tamisemi,George Simbachawene na aliyeko kulia kwake ni mkuu wa mkoa wa Arusha Daud Filex Ntibenda,wakiwa katika kilele cha sikukuu ya nanenane,katika viwanja vya Themi Njiro Jijini Arusha.
Mkuu Mkoa wa Arusha Daud Filex Ntibenda akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadick wakiwa wanamtunza mmoja wa waimbaji wa ngoma ya kipemba katika viwanja vya Taso Themi Njiro (hao vijana ni wa JKT  Oljoro).
Waziri wa Nchi Ofisi ya rais ,Tamisemi akiwa na akiwa wanamtunza mmoja wa waimbaji wa ngoma ya kipemba katika viwanja vya Taso Themi Njiro,katika kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya wakulima na wafugaji nanenane ,  (Ngoma hiyo ni ya vijana kutoka JKT  Oljoro).




No comments