Askari wa Upelelezi Mwanza Auawa Baa......6 Watiwa Mbaroni, RPC Msangi Anena
Kwamba tarehe 21.08.2016 majira ya 10:00 usiku katika eneo la club ya villa
park resort kata ya kirumba wilaya ya ilemela mkoa wa mwanza, askari namba
g.5092 pc john nyange wa ofisi ya mkuu wa upelelezi na makosa ya jinai mkoa
wa mwanza (rco), aliuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali eneo la
shingoni na mtu aliyekuwa anaugomvi nae.
Inadaiwa kuwa marehemu alikua na ugomvi wa muda mrefu na mtu
aliyejulikana kwa jina magina hussein miaka [27] fundi computer msukuma na
mkazi wa mtaa wa kigoto, ambapo marehemu alikuwa akimdai bwana magina
hussein computer aina ya laptop. Ndipo usiku wa leo majira tajwa hapo juu
walikutana eneo la club ya villa park huku mtuhumiwa wa mauaji hayo
ikisemekana kuwa alikuwa na wenzake watano ndipo walimvamia na
kumchoma na kitu chenye ncha kali shingoni na kufariki dunia njiani wakati
akipelekwa hospitali.
Marehemu kwa sasa alikuwa ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha stefano moshi
memorial university college cha mjini moshi, alikuwa anasomea shahada ya
sayansi ya habari na mawasiliano mwaka wa pili, aidha alirejea mwanza baada
ya kupata likizo kuja kuiangalia familia yake ndipo umauti ukamkuta.
Watuhumiwa sita akiwepo magina selemani ambaye alikuwa na ugomvi na
marehemu pamoja na wenzake watano wamekamatwa, wapo katika mahojiano
na jeshi la polisi huku uchunguzi kuhusiana na kifo hicho ukiwa bado
unaendelea, pindi uchunguzi ukikamilika watuhumiwa wote watafikishwa
mahakamani, mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya rufaa ya bugando
kwa uchunguzi.
Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza naibu kamishina wa polisi ahmed msangi
anatoa wito kwa wananchi wa jiji na mkoa wa mwanza, kwamba jeshi la polisi
mkoa wa mwanza limesikitishwa na kifo cha askari huyu kwani limempoteza
askari kijana ambaye bado jeshi lilikuwa linamtegemea.
Lakini pia anawataka watu wenye tabia za kujichukulia sheria mkononi kwa
kuwapiga wengine hadi kufikia kupoteza maisha kuwa wanafanya kosa la jinai,
na kama watu wanadaiana wafuate taratibu za kisheria zilizowekwa ili
kuepusha vifo vinavyoweza kuepukika, hivyo jeshi la polisi linawataka kuacha
tabia hiyo mara moja kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Imetolewa na:
Dcp: ahmed msangi
Kamanda wa polisi (m)Mwanza
No comments