Jella Mambo:Tunaunga mkono Ukuta Septemba mosi.
Kamati Kuu ya Chadema wakishikana mikono kuonyesha mshikamano.
CHAMA cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kanda ya kati kimesema kuwa kinaunga mkono azimio la Kamati kuu ya chama hicho ya operesheni Umoja wa Kupambana na Udiktete Tanzania (UKUTA) Septemba Mosi mwaka huu.
Jella Mambo ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Dodoma akizungumza na waandishi wa habari leo juu ya maandalizi ya kufanyika kwa maandamano hayo pamoja na mikutano ya hadhara.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo akadai kuwa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania inavunjwa na baadhi ya viongozi wa serikali ya awamu ya tano
Aidha Mambo akaviita vitendo hivyo kuwani chanzi cha ubaguzi kwa vyama vya siasa.
Pia chama hicho mkoa wa Dodoma wamelaani vikali vitendo vya jeshi la polisi kuwasumbua wanachama wake wakiwemo wanafunzi wa vyuo vikuu, jeshi la polisi limekuwa likiwakamata hovyo kuwabambikia kesi wanachama huku chama hicho kikidai vitendo hivyo vimekuwa vikiwanyima muda wa kufanya kazi za maendeleo.
Aidha kauli hiyo ya viongozi wa chama cha democrasia na maendeleo chadema inakuja wakati vyombo vya usalama nchini chini ya agizo la rais kutofanyika maandamano vimepiga maraufuku mikutano yoyote ambayo imepangwa na chama hicho mwanzoni mwa mwezi ujao.

No comments