Godbless Lema Apandishwa Mahakamani.......Aachiwa Kwa Dhamana
Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema amepandishwa mahakamani katika
kesi mbili tofauti.
Kesi ya kwanza namba 351/2016 anatuhumiwa kumtumia ujumbe wa simu wa
uchochezi Mkuu wa mkoa Arusha, Mrisho Gambo wenye maneno kuwa “Karibu
tutakudhibiti kama mashoga walivyodhibitiwa Uarabuni”
Kesi ya pili namba 352/16 Lema anatuhumiwa kuhamasisha maandamano
Septemba Mosi kinyume cha sheria.
Hakimu amepinga hoja za wakili wa Serikali, Vincent Njau kuzuia dhamana
kwa sababu za kiinterejensia kwa usalama wake.
Lema amekana mashitaka yote, na ameachiwa kwa dhamana baada ya
kutimiza masharti ambapo kwa shitaka la kwanza alitakiwa kupata mdhamini
na shilingi 10, na shitaka la pili dhama ni shilingi milioni 15.Kesi hiyo itatajwa
tena Septemba
Hakimu anayesikiliza kesi ni Desderi Kamugisha wakati wakili wa serikali akiwa
ni Innocent Njau.
Baadaye vurugu ziliibuka mahakamani wakati polisi wanataka kumpeleka Lema
magereza kwa madai kuwa wadhamini wamechelewa, lakini mbunge huyo
alipinga hatua hiyo kwa maelezo muda wa mahakama saa 9.30 ulikuwa bado.
Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema akiwa amepakatiwa na mkewe baada ya kuachiwa kwa dhamana kwa kesi inayomkabili mahakama ya hakimu mkazi.Pichani akiwa hoi baada ya kushinda njaa kwa siku mbili akidai kufunga kwa kushinda na njaa kwaajili ya kuombea taifa
.
Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema akiwa hospitalini baada ya kutoka mahakamani na kusomewa mashtaka nakutajiwa makosa yake 1.kwanza likiwa ni kitoa lugha ya matusi yakumtukana mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Ghambo, 2.kufanya uchochezi kwa njia ya sauti na kuchochea maandamano yasiyokuwa halali ya septemba mosi.

No comments