DC Karatu :Waandishi wa habari kuweni wazalendo kwa nchi yenu,
Mkuu wa wilaya ya Karatu akizungumza na waandishi wa habari Katika mkutano mkuu wa mwaka .Picha kwa idhini ya APC.

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari mkoani Arusha Cloud Gwandu akizungumza katika mkutano huo.Picha kwa idhini ya Apc.

Mkuu wa wilaya ya Karatu Theresia Muhongo akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya uongozi wa chama cha waandishi wa habari mkoani Arusha.picha kwa niaba ya Apc.
Mkuuwa wilaya ya Karatu Theresia Muhongo akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari mkoani Arusha walipotembelea wilaya ya Karatu.Picha kwa idhini ya APC.
MKUU wa Wilaya ya Karatu, Theresia Mahongo amewataka waandishi wa habari kuwa wazalendo kwa nchi yao na kuepuka kutumia kalamu zao kuingiza nchi katika machafuko.
Aidha wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (APC), wameutaka uongozi wa chama hicho kutoa wiki mbili au kurudisha pikipiki mbili zilizotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kwaajili ya kujipatia fedha lakini hadi leo hakuna kadi ya umiliki wa pikipiki hizo.
Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Wilaya Karatu, Mahongo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa wanachama.
Alisema waandishi wa habari ni watu muhimu kwa jamii lakini ni vyema sasa wanahabari kuwa wazalendo na kuandika habari zinazoleta manufaa na kujiepusha na kuingiza masuala ya siasa.
"Ishi kesho, msilete mchafuko zingatieni maadili habarisheni umma kwa maendeleo ya taifa letu na vizazi vyetu lakini pia nasisitiza mtangaze vivutio vya utalii kwani Tanzania inafursa nyingi za vivutio vya utalii,"alisema
Akitolea mfano alisema siku ya tukio la kupigwa risasi Tundu Lissu baadhi ya mitandao ya jamii iliandika amepigwa risasi tano na kufa hapo hapo.
"Nilikuwa katika mwenye niliposikia hali ilikuwa tofauti watu wote tulishikwa na but wasiwasi,kuja kifungilo kumbe majeruhi na hadi sasa mzima, hivyo nyie ndio wakuhabarisha jamii acheni kukurupuka kuandika vitu msivyokuwa nacho uhakika ili tudumishe amani,"alisema
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Waziri Morice alitoa rai kwa kutokubali kutenganishwa kwa namna yoyote ile bali kuandika habari zenye tija na kuibua maendeleo katika wilaya mbalimbali za Mkoa wa Arusha.
Naye Mwenyekiti wa APC, Mkoa wa Arusha,Claud Gwandu alikiri ni kweli pikipiki hizo zilitolewa miezi zaidi ya nane iliyopita lakini hadi leo kila wakifuatilia usajili wa pikipiki hizo ikiwemo kadi zake wanazunguushwa hapo Mkoani hali inayoibua maswali mengi kwa wanachama.
Kutokana na maazimio ya wanachama wa Apc katika mkutano huo mkuu, wanachama kwa sauti moja walitoa wiki mbili kwa uongozi wa Apc kuuliza hizo kadi za pikipiki zimefikia wapi na kama hakuna jambo lolote litakaloendelea baada ya wiki mbili zirudishwe .
"Wacha tusubiri wiki mbili ziishe na pia tuonane na RC
Mrisho Gambo ili kumweleza vikwazo tulivyokutana navyo na kama ndani ya wiki mbili hakuna utaratibu wowote tutazirudisha, " alisema
Kuhusu miradi ya klabu, Naibu Katibu Mkuu wa APC, Mustafa Leu alisema APC ipo kwenye mchakato wa kukamilisha kiwanja kilichopo eneo la Oljoro kilichopewa na Halmashauri ya Jiji la Arusha na baada ya mchakato wa upimwaji viwanja kukamilika hati itatolewa ili Apc iamue kujenga jengo lake na kujikwamua kiuchumi


No comments