CHODETA AISHAURI KAMISHENI KUAJIRI WATAALAM


Kaimu mkurugenzi wa miundo mbinu na huduma za jamii kutoka wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Eliabi Khalid Chodeta 

Na.Vero Ignatus, Zanzibar.

Kaimu mkurugenzi wa miundo mbinu na huduma za jamii kutoka wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Eliabi Khalid Chodeta ameishauri Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki kupeleka barua wa baraza la mawaziri Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kujadili suala la kuongeza wafanyakazi.




Wa kwanza kushoro ni Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Kiswahili Afrika ya Mashariki Profesa Kenneth Simala.Picha na Vero Ignatus Blog.

Awali Katibu Mtendaji wa jumuiya hiyo Profesa Kenneth Simala amesema suala la kuajiri kwenye jumuiya hiyo linamchakato mrefu kutokana na kutakiwa kuajili nafasi chache za juu.

Mtendaji huyo aliongeza kuwa kwa ujumla kamisheni hiyo inatakiwa kuwa na wafanyakazi 31.

Kwa upande wake,Chodeta alisisitiza kuwa ni muhimu kwa kamisheni hiyo kuajiri wataalamu ili kuanza mara moja shughuli xake ikiwapo kutoa semina.



No comments