WAKUU WA VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII WAENDELEA NA MAFUNZO KUHUSU UDHIBITI WA VIASHIRIA HATARISHI KATIKA UTENDAJI WA VYUO MKOANI MOROGORO
Mkuu
wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Mwenyekiti wa Mafunzo Bw. Paschal
Mahinyila akiwakaribisha washiriki katika mafunzo Wakuu wa vyuo hao
kuhusu Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo
yanayofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti mkoani Morogoro
leo tarehe 01.08.2017.
Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike (kushoto) akifafanua umuhimu
wa uadilifu kwa Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii(hawapo pichani)
katika utendaji kazi wa vyuo wakati wa mafunzo kwa wakuu wa vyuo hao
kuhusu Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Uendeshaji wa Vyuo hivyo
yanayofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro
leo.
Mkurugenzi
wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii
Jinsia Wazee na Watoto Bibi Deodata Makani(kulia) akifafanua mambo
mbalimbali ya kiutawala kwa Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini
katika mafunzo kwa wakuu wa Vyuo hao kuhusu Udhibiti wa Viashiria
Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika ukumbi wa
Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro leo.
Mhasibu
Mkuu kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto
Bibi Fatuma Oloo(kulia) akisisitiza jambo kuhusu udhibiti wa fedha kwa
wakuu wa vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini katika mafunzo kwa wakuu wa
vyuo hao kuhusu Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo
hivyo yanayofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani
Morogoro.
Mkurugenzi
wa Ugavi na Manunuzi kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia
Wazee na Watoto Bibi Martha Chuma (katikati) akifafanua mambo mbalimbali
yahusuyo ugavi na manunuzi kwa wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii
nchini katika mafunzo kwa wakuu wa Vyuo hao kuhusu Udhibiti wa Viashiria
Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika ukumbi wa
Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro.
Mkuu
wa Kitengo cha Sheria kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia
Wazee na Watoto Bi. Vickness Mayao(kulia) akitoa maelekezo kuhusu
mikataba na masuala mbalimbali ya kisheria kwa wakuu wa vyuo vya
Maendeleo ya Jamii nchini katika mafunzo kwa wakuu wa Vyuo hao kuhusu
Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo
yanayofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro.
Mkaguzi
wa ndani kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na
Watoto Bibi. Elightness Mchome(katikati) akifafanua umuhimu wa kuepuka
hoja za ukaguzi kwa wakuu wa vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini katika
mafunzo kuhusu Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo
hivyo yanayoendelea katika ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani
Morogoro.
Mkuu
wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Monduli Bw. Salim Mgalla(kulia) akiuliza
swali kwa wawezeshaji katika mafunzo kwa wakuu wa vyuo vya Maendeleo ya
Jamii nchini katika mafunzo kwa wakuu wa vyuo hao kuhusu kuhusu Udhibiti
wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika
katika ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro
Baadhi
ya wakuu wa vyuo vya Maendeleo ya Jamii Nchini wakifuatilia
wawasilishaji mada(hawapo pichani) katika mafunzo kwa wakuu wa vyuo hao
kuhusu Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo
yanayofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro.
Mratibu
wa Usimamizi wa Viashiria Hatarishi Bw. Moris Jackson akifafanua
masuala mbalimbali yahusuyo Viashiria Hatarishi kwa wakuu wa vyuo vya
maendeleo ya Jamii Nchini katika mafunzo kwa wakuu wa vyuo hao kuhusu
Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo
yanayofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro.
Kaimu
Mkuu wa Chuo (Utawala, Mipango na Fedha) Kutoka Chuo cha Maendeleo ya
Jamii Ruaha Bi.Nadhaherieth Mshighath akiuliza swali kwa wawasilishaji
mada (hawapo pichani) katika mafunzo kwa wakuu wa vyuo hao katika
mafunzo kwa wakuu wa vyuo hao kuhusu Udhibiti wa Viashiria Hatarishi
katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika ukumbi wa Wakala wa
Mbegu za miti, mkoani Morogoro.
Watendaji
kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na
washiriki kutoka Vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini wakifuatilia kwa
makini mafunzo ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa
Vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini yanayofanyika katika ukumbi wa Wakala
wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro leo 01.08.2017.
Picha na Erasto Ching’oro WAMJW.
No comments