WAKULIMA WAHIMIZWA KUTUMIA RASILIMALI ZA NCHI KWA KULIMA KILIMO CHA UMWAGILIAJI
Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo Ndg Methew J. Mtigumwe akisoma na kupata maelezo
mbalimbali kuhusu ufanisi katika Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) mara
baada ya kutembelea banda hilo wakati wa Maonesho ya Nanenane katika
Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo Ndg Methew J. Mtigumwe akisikiliza maelezo ya namna
ya ufyatuaji matofali yanayotumika kujengea nyumba za NHC mara baada ya
kutembelea banda hilo wakati wa Maonesho ya Nanenane katika Viwanja vya
Ngongo Mkoani Lindi.
Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo Ndg Methew J. Mtigumwe (Kushoto) akisikiliz akwa
makini maelezo kuhusu ufanyaji kazi katika banda la TAMISEMI mara baada
ya kutembelea banda hilo wakati wa Maonesho ya Nanenane katika Viwanja
vya Ngongo Mkoani Lindi. Mwingine ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mkoani
Lindi Mhe Rukia Muwango.
Mkurugenzi
wa maendeleo ya mazao Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi idara kuu ya
kilimo Ndg Twahir Nzallawahe akisikiliza maelezo mbalimbali katika banda
la Nanyamba mara baada ya kutembelea banda hilo wakati wa Maonesho ya
Nanenane katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Mkurugenzi
wa maendeleo ya mazao Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi idara kuu ya
kilimo Ndg Twahir Nzallawahe akisikiliza maelezo mbalimbali katika banda
la Nanyamba mara baada ya kutembelea banda hilo wakati wa Maonesho ya
Nanenane katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi. Mwingine ni Mkuu wa
Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi.
Lindi
Pamoja
na mazao mbalimbali yanayolimwa na wakulima nchini Tanzania lakini
wametakiwa kujikita zaidi na kilimo cha mazao yanayostahimili ukame
ikiwemo kuanzisha kilimo cha umwagiliaji hususani katika maeneo yaliyopo
pembezoni mwa Bahari ya Hindi katika Mikoa ya Mtwara na Lindi.
Kufanya
hivyo ni kutumia vizuri rasilimali za nchi ikiwemo maji na maeneo oevu
katika kilimo chenye tija jambo ambalo linatoa fursa kwa wakulima wadogo
kuwa na kipato kikubwa na kutafsiri ipasavyo kipato cha nchi na mtu
mmoja mmoja.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa maendeleo ya mazao Wizara ya Kilimo
Mifugo na Uvuvi idara kuu ya kilimo Ndg Twahir Nzallawahe alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo Ndg Methew J. Mtigumwe mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali
ya Maonesho ya Nanenane katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Nzallawahe
alisema kuwa katika mikoa ya Mtwara na Lindi serikali tayari imeanzisha
kanda ya umwagiliaji ambapo kuna mradi wa Kitele huku akisema kuwa
jitihada zaidi za kuwa na miradi ya umwagiliaji katika mikoa yote nchini
zinaendelea.
Alisema
kuwa pamoja na mbinu bora za Kilimo Mifugo na Uvuvi wanazopatiwa
wananchi lakini pia Maonesho ya Nanenane kwa mwaka huu 2017 yamezidi
kuwa bora zaidi ukilinganisha na Maonesho ya kipindi cha miaka miwili
iliyopita.
Aliongeza
kuwa wananchi wanapaswa kutembelea katika Maonesho hayo ili kujifunza
mbinu mbalimbali za Kilimo Mifugo na Uvuvi huku akiwasisitiza zaidi
kununua bidhaa zinazotengenezwa na kuzalishwa ndani ya nchi kwani
kufanya hivyo watarahisisha kipato cha wakulima nchini ikiwemo pia
kurahisisha kasi ya ukuaji wa kilimo.
Aidha
amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe
Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya nchini hususani kuwapatia wananchi
maeneo kwa ajili ya kilimo.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi Mhe Rukia Muwango alisema
kuwa Katika Maonesho haya wakulima watajifunza mbinu bora za kisasa za
kilimo zitakazowawezesha kupata mazao mengi na kuinua kipato chao.
Aidha
ametoa wito kwa wakulima na mashirika kujitokeza katika maonesho hayo
kwa sababu watapata fursa ya kujifunza mambo mengi na kubadilishana
uzoefu na wataalamu mbalimbali wa kilimo.
No comments