MAMLAKA YA MAWASILIANO NCHINI TCRA IMETOA ELIMU KWA WATUMIAJI WA MAWASILIANO HUDUMA NAMNA YA KUHAMA MTANDAO MWINGINE WA SIMU BILA KUBADILI NAMBA YA SIMU YA KIGANJANI
![]() |
| Injinia Jan Kaaya akiwa anamfanfanulia jambo mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira kama inavyoonekana pichani katika maonyesho ya nanenane mkoani Arusha |
Pichani Meneja wa TCRA kanda ya kaskazini Injinia Annette Matindi akiwa na wafanyakazi wengine wa TCRA wakitoa elimu kama wanavyoonekana pichani.Picha na Vero Ignatus Blog.

Injinia Jan Kaaya akiwa anafurahia jambo mara baada ya kumuhudumia mteja katika maonyesho ya nanenane (haonekani pichani)yanayoendelea katika viwanja vya Themi Njiro mkoani Arusha .Picha na Vero Ignatus Blog
Injinia Jan Kaaya akiwa anafurahia jambo mara baada ya kumuhudumia mteja katika maonyesho ya nanenane (haonekani pichani)yanayoendelea katika viwanja vya Themi Njiro mkoani Arusha .Picha na Vero Ignatus Blog
Afisa Oswad Octavian kutoka TCRA kanda ya kaskazini akitoa elimu kwa mteja alipotembelea katika banda lao katika maonyesho ya nanenane mkoani Arusha .Picha na Vero Ignatus Blog.
Mhandisi masafa kutoka TCRA Julius Felix alitoa elimu kwa wateja aliotembelea banda la Mamlaka hiyo katika maonyesho ya nanenane katika viwanja vya Themi Njiro Mkoani Arusha.Picha na Vero Ignatus Blog.
Na.Vero Ignatus ,Arusha.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya huduma mpya ya kuhamia mtandao mwingine bila kubadili namba ya simu ya kiganjani (MNP-Mobile Number Portabilitty service) ambapo namba ya kitambulisho itakuwa
namba mtumiaji
Huduma
hii ilianza tarehe mosi machi 2017 na inapatikana nchi nzima kwenye maduka ya kutolea huduma kwa wateja wa mitandao ya makampuni yote ya simu za kiganjani
Huduma hiyo ya kuhama mtandao mwingine bila ya kubadili namba yako na mtumiaji
anabakia na namba kumchagua mtoa huduma
bora zaidi ,atapokea ujumbe mfupi wa maneno bila
kujali ni mtandao upi umehamia, itamuepushia usumbufu wa
kununua laini mpya mara kwa mara
Namna
ya kuhama mtandao bila kubadili namba ya simu kiganjani,ili kuingia
kwenye mfumo huu simu ya mtumiaji lazima iwe inatumika yaani
haijafungiwa au kusimamishwa kwa muda.
MASHARTI YA KUHAMA
Ili uweze kutumia huduma hii ,inabidi kuzingatia masharti yafuatayo:
a)Hutaweza kuhama na namba ambayo imefungwa ama kusimamishwa huduma
b)Hutaweza
kuhama na salio lililopo itabidi utumie salio kabla ya kuhama la sivyo
salio lako litatunzwa kwenye akaunti maalumu ya mtoa huduma wako wa
zamani na utalazimika kufuata taratibu za kudai ili urudishiwe.
C)Huwezi kuhama kama unamkopo wa aina yeyote ile(muda wa maongezi au pesa mtandao )kutoka kwa mtoa huduma wako hapa nchini.
D)Huwezi kuhama kama namba yako inahusishwa na uhalifu na imefungiwa
Tcra:
Iwapo unatumia huduma kwa utaratibu wa malipo baada ya huduma yaani
post-paid:zingatia mashrti yaliyotajwa hapo juu ya wateja wa pre-paid na
masharti mengine yafuatayo;
a)Itabidi ulipe madeni yote kabla ya kuhama
b)Itabidi
ukamilishe mashrti ya msingi ya mkataba na mtoa huduma wako
wa sasa na
kutimiza masharti ya malipo kila mwezi kwa mujibu wa mkataba kabla ya
kuhama
C)Utaendelea
kupokea ankra za matumizi hadi namba itakapokamilishwa kwa mtoa huduma
mpya .
Utapokea ankra ya mwisho hadi siku 60 baada ya kuhamisha namba yako kisha unapewa mpaka siku 30 za kulipa ankra hizo vinginevyo utakuwa katika hatari ya uhamaji wako utasitishwa au namba yako kufungiwa,
Utapokea ankra ya mwisho hadi siku 60 baada ya kuhamisha namba yako kisha unapewa mpaka siku 30 za kulipa ankra hizo vinginevyo utakuwa katika hatari ya uhamaji wako utasitishwa au namba yako kufungiwa,
UTARATIBU WA KUHAMA
1.Tembelea
vituo vya mauzo au kwa wakala anayetambuliwa wa mtoa huduma unakokataka
kuhamia na umueleze mhudumu kwamba ungelipenda kuhama na namba yako.
2.Mhudumu atakutaka ujaze fomu maalum ya maombi
3.Sehemu
ya fomu ya maombi ya kuhama ni tamko rasmi kwamba unakubali kuwa
unawajibika kuwa madeni yote ambayo yanatokana na huduma ulizokuwa
unapata kutoka kwa mtoa huduma wako wa awali
4.unatakiwa kutoa vifuatavyo:
a)Kitambulisho
chenye picha yako kinaweza kuwa kitambulisho cha Taifa Kadi ya mpiga
kura leseni ya udereva au pasipoti au kitambulisho chochote rasmi
kinachotambulika
b)Simu ya kiganjani inayofanyakazi yenye namba unayotaki kubaki nayo
5.Iwapo
una salio katika akaunti ya pesa mtandao unashauriwa kutoa pesa kabla
ya kuhama ili kuepusha usumbufu baada ya kuhama mtandao mwingine.
6.Utatakiwa
kutuma meseji yenye neno HAMA" kwenda namba 15080 ambaoyo ni namba
maalum ya kuhama.msaada utatolewa iwapo utahitjikq ili kufanikisha
hili.
7.Utapokea meseji kukujulisha kwamba maombi yako yamepokelewa
8.Iwapo
namba yako haikuzuiliwa au kusimamishwa kwa muda kutokana
na
kutokukamilisha malipo ya madeni ya mtoa huduma wako wa awali maombi
yako yatashughulikiwa na utakulishwa kwa meseji kuhusu maendeleo ya
mchakato huu
9.Mtoa huduma wako mpya wa huduma za simu ya kupiga na kupokea na ujumbe mfupi zitaendelea kama kawaida
10.Ili
kupokea mihamala ya fedha mtandao wakati wa kuhama ,huduma za kifedha
zitasitishwa kwa muda mpaka namba itakapokamilishwa kwa mtoa huduma mpya
ambapo utatumia huduma zake za fedha mtandao kama utajiunga na huduma
zipo.
11.Katika kipindi chq kuhama huduma za kupiga na kupokea na ujumbe zitaendelea kama kawaida
12.Katika
hali ya kawaida uhamaji utakamilika haraka mara nyingi siku hiyohiyo
au iwapo utachelewa sana,ndani ya siku mbili za kazi baada ya
kukamilisha utaratibu wa maombi.wakati huo namba yako utakuwa
umeshahamishwa kwa mtoa huduma wako mpya na laini
13.Ikifikia
hapo weka laini mpya uliyopewa na mtoa huduma wako mpya kwenye simu
yako ,iwapo huna uhakiki wa nn cha kufanya unaweza kwenda kwa mtoa
huduma au wakala au kuwapigia simu na wataweza kuusaidia.
14.Mchakato umekamiliaka



No comments