Tetemeko kubwa lakumba kusini magharibi mwa China
Tetemeko hilo lilisikika Xian, umbali wa mamia ya kilomita
Tetemeko la ardhi
la ukubwa wa 7.0 katika vipimo vya richa limesababisha vifo va takriban
watu 13 na kuwajeruhi kadha kwenye mkoa ulio kusini mashariki mwa nchi
wa Sichuan.
Tetemeko hilo lilikumba eneo lisilo na watu kusini mwa mkoa wa Sichuan.Baadhi ya ripoti zinasema kuwa huenda idadi ya waliokufa ikaongezea. Kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa eneo lililo maarufu kwa watalii.

Mmiliki mmoja wa hoteli alisema kuwa tetemeko hilo lilikuwa na nguvu kuliko lile la mwaka 2008.

Rais Xi Jinping alitaka jitihada zote kufanywa na kuokoa watu waliojeruhiwa.

No comments