RAIS MAGUFULI AMTEUA JENERALI VENANCE MABEYO KUWA MKUU WA MAJESHI YA ULINZI TANZANIA
Jenerali Venance Mabeyo
Rais John Magufuli amemteua Luteni Jenerali Venance Mabeyo kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania.
Taarifa ya Ikulu jijini Dar es Salaam imesema pamoja na kuteuliwa kuwa
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Luteni Jenerali Mabeyo amepandishwa
cheo na kuwa Jenerali.
Jenerali Mabeyo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali Davis Mwamunyange ambaye amestaafu.
Wakati huo huo Rais Magufuli amemteua Meja Jenerali James Mwakibolwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania.
Taarifa hiyo imesema pamoja na kuteuliwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi
ya Ulinzi Tanzania Meja Jenerali Mwakibolwa amepandishwa cheo na kuwa
Luteni Jenerali.
Luteni Jenerali Mwakibolwa anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali
Mabeyo ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania.
No comments