Mwanariadha afia getini Kili Marathon

Mwanariadha,
Charles Maroa kutoka nchini Kenya amefikwa na maut katikahospitali ya
KCMC mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro, baada ya kuanguka katika geti la
viwanja vya Ushirika wakati alipokuwa akielekea kumaliza mbio za nusu
Marathon za Kilimanjaro zilizofanyika jana Februari 26.
Akithibitisha
kutokea kwa kifo hicho kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kilimanjaro, RPC Raymond Mtafungwa alisema kuwa Mwanariadha huyo
alikutwa na umauti huo jana majira ya saa tano asubuhi katika hospitali
la KCMC mjini Moshi baada ya kuanguka.
"Tumepokea
taarifa za kifo cha Mwanariadha huyo alietambulika kwa jina la Charles
Maroa,ambaye ni raia wa Kenya (Mkurya), baada ya kukumbwa na hali hiyo
alikimbizwa hospitali ya KCMC kupatiwa huduma ya kwanza baada ya
kuanguka ghafla katika geti kuu la kuingia katika viwanja vya Ushirika
hapa mjini Moshi wakati alipokuwa akielekea kumaliza mbio za nusu
Marathon za Kilimanjaro na tunaendelea na uchunguzi kujua nini kilitokea
mpaka kuelekea kifo chake" alisema.
Mwili wa Mwanariadha huyo umehifadhiwa katika hospitali ya KCMC mjini Moshi.
No comments