SERIKALI YAOMBWA KUONDOA TOZO YA KODI KWA WAUZAJI WADOGOWADOGO WA TANZANITE
Na.Vero Ignatus ,Arusha.
Serikali imeombwa iwafikirie wauzaji wadogowadogo
wa madini ya Tanzanite mkoani Manyara na Arusha , kwenye ulipaji wa tozo ya kodi kwa asilimia 18 kwani kodi
hiyo inalengo la kuwamaliza wafanyabiashara wadogowadogo wa madini hayo.
Akizungumza
kwenye mnada wa vito wa madini ya Tanzanite, Mwenyekiti wa mabroka
mkoa wa Arusha,Jeremia Simioni alidai licha ya kodi kuwa kihalali
kisheria lakini ni wazawa pekee ndio wanaotakiwa kulipa kodi hiyo
Alisema
ipo sababu ya serikali kukangalia namna ya ulipaji wa kodi hiyo,aidha
kuiondoa kabisa ama na wafanyabiashara wageni nao wakapangiwa namna ya
kulipa kodi hiyo
"Utamkuta mfanyabiashara
ananunua mawe 50 milioni na anaekewa VAT kwa asilimia 18 au zaidi chakushangaza mgeni atanunua mawe kwa kiasi hicho au zaidi lakini hatozwi VAT
hiyo,"alisema Jeremia
"Sasa jamani inakuaje mzawa alipe kodi lakini mgeni asilipe kodi yeye anafanya biashara kama ni bure kwakweli serikali ilitizame hili sasa, "alisema Jeremia
Hata
hivyo alisema pamoja na serikali kudai kuwarudushia baadhi ya malipo
hasa kwa wafanyabiara wanaosafirisha madini hayo bado utekelezaji huo
haujaanza
"Hajawahi kulipwa mtu,sisi tunataka aidha tozo iondolewe ama tulipe wote ,"alisema Jeremia
Sambamba na hayo ameiomba serikali iwaandalie mnada wafanyabishara wa madini wadogowadogo ili nao waweze kukua kwenye biashara hiyo
"Mnada
mzuri lakini huwezi kuchanganya wafanyabiashara wakubwa na wadogo,sisi
tunaiomba serikali iandae mnada kwaajili ya wafanyabaishara wa madini
wadogowadogo,"alisema Jeremia
Mbunge wa Simanjiro,James Olemilia ameitaka serikali kuhakikisha mjinj wa Manyara unapotokea madini ya tanzanite unakua
"Simanjiro
pamoja na kuwa linatoa madini ya tanzanite ambayo yanategemewa na
mataifa mbalimbali lakini bado maisha magumu,hakuna Zahanati,shule
,tunataka madini hayo yainufaishe kwanza simanjiro,"Alisema James
Mkuu
wa mkoa wa Manyara Joel Bendera alidai ipo sababu ya serikali
kuangalia namna ya kuhakikisha wachimbaji wadogowadogo wa madini
wananufaika
Amesema kuwa Mkoa wa Manyara haswa Simanjiro ni mkoa ambao unaongoza kwa maambukizi virusi vya ukimwi pamoja na TB
"Afya
wa wachimbaji lazima izingatiwe ni asilimia 19 ya wakazi wa manyara
wanavirusi vya ukimwi,tb iko juu sana ,"alisema Bendera
Hata
hivyo kutokana na mnada huo,Mkurugenzi wa TANSORT Arichad Kalugendo,
alisema faida ya marabaha yaliyouzwa ni 9 bilioni,huku serikali ikopokea
tuzo kwa zaidi ya 400 milioni huku wilaya ya simanjiro ikinufaika kwa
kiasi cha shilingi 26 milioni
No comments