MAKALA YA MAANDALIZI YA SIKU YA WANYAMAPORI DUNIANI 3/3/2017
Bw. Malima Mbijima akizungumza
na wananchi wa kijiji cha Chisingisa
TAWA
wakishirikiana na Mradi wa kuhimarisha Mtandao wa Maeneo
Yaliyohifadhiwa Kusini mwa Tanzania (SPANEST), kwa kutumia wataalamu
wake, inafanya ziara ya kutembelea vijiji vinavyozunguka Pori la Akiba
Rungwa katika Wilaya ya Manyoni kwa kutoa elimu ya wanyamapori kwa njia
za mikutano kufuatia maandalizi ya Siku ya Wanyamapori Duniani ambayo
yanategemewa kuadhimishwa jijini Dar es Salaam tarehe 3/3/2017. Kauili
mbiu ya Siku ya Wanyamapori Duniani ni ‘Vijana tushiriki katika
Uhifadhi’
Elimu
hii katika Wilaya ya Manyoni imeanza rasmi tarehe 18/2/2017 na
itachukua muda wa siku kumi na kuhitimishwa tarehe 25/2/2017
inawashirikisha wataalamu wa Maliasili kutoka wilaya ya Manyoni
wakiwemo Afisa Misitu na Afisa wanyamapori wa Wilaya ya Manyoni.
Vijiji vilivyoelimishwa ni kijiji cha Imalampaka, Sasilo na Ipululu.
Vijiji vingine ambavyo vimelengwa kuelimishwa ni Simbanguru, Mpapa,
Iseke,Nkonko,Damwelu,Doroto na Lulanga.
Msafara
huo unaongozwa na Bw. Twaha Twaibu ambaye ni Afisa habari na Mahusiano
wa TAWA ambaye ameongozana na Bw. Herman Nyanda naye kutoka TAWA
anayeshughulikia Ushirikishwaji jamii katika uhifadhi, Bw. Ramadhani
Mdaile kutoka Pori la Akiba Rungwa nayeshughuka na Masuala ya Uenezi,
Bw. Malima Mbijima kutoka mradi wa SPANEST na wataalamu wa maliasili
kutoka Wilaya ya Manyoni.
Bw. Twaha Twaibu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Imalampaka
Kwenye
mikutano hiyo, Bw. Twaha aliwaelezea wananchi wa vijiji hivyo faida
mbalimbali zitokanazo na uhifadhi wa wanyamapori, Sheria ya kuhifadhi
wanyamapori Na.5 ya Mwaka 2009, suala la wanyamapori wakali na
waharibifu, utaratibu wa kufuata na jinsi Serikali inavyowalipa wananchi
wake kifuta jasho na machozi baada ya mashamba yao kuharibiwa na
wanyamapori na wengine kujeruhiwa au kuuwawa na wanyamapori.
Aliwaeleza kuwa Serikali yao kupitia Wizara ya Malaisili na Utalii inawajali sana na kuwaomba wasijihusishe na vitendo vya ujangili wa wanyamapori,
Aliwaeleza kuwa Serikali yao kupitia Wizara ya Malaisili na Utalii inawajali sana na kuwaomba wasijihusishe na vitendo vya ujangili wa wanyamapori,
Aidha
mtaalam kutoka mradi wa SPANEST Bw. Malima Mbijima alieleza kwamba
mradi huo unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania na
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) ukiwa na lengo la
kuendeleza uhifadhi wa wanyamapori katika ukanda wa kusini mwa Tanzania
unao jumuisha Pori la Akiba la Rungwa, Pori la Akiba Mpanga Kipengele,
Hifadhi ya Taifa Ruaha na Kitulo, ili wanyamapori hao waweze kuchangia
zaidi maendeleo ya jamii katika kizazi cha sasa na vijavyo kupitia
utalii na fursa nyingine. Shughuli za Utalii hapa Tanzania zinachangia
asilimia 25 ya fedha za Kigeni.
Wananchi wa kijiji cha Imalampaka wakiwa kwenye picha ya pamoja
Bw.
Ramadhani Mdaile akisisitiza suala la kutojihusisha na ujangili wa
wanyamapori na ukataji wa mbao katika Pori la Akiba, aliwaeleza wananchi
kuheshimu mipaka ya Hifadhi ya Mapori ya Akiba kwa kuacha mita 500
kutoka hifadhi wanapolima au kufanya shuguli zao.
Mita hizi ziko kisheria kwa kuzingatia Sheria ya Kuhifadhi wanyamapori Na.5 ya mwaka 2009.
Bw.
Herman Nyanda kutoka Makao Makuu ya TAWA aliwaeleza wananchi kuhusu
faida na umuhimu wa kuanzisha maeneo ya hifadhi za wanyamapori (WMAs)
katika maeneo yao ya vijiji. Uanzishaji na utunzaji wa maeneo ya hifadhi
za wanyamapori ni njia mojawapo ambayo itawawezesha wananchi kunufaika
na uhifadhi wa wanyamapori kupitia shughuli za uwindaji wa kitalii na
utalii wa picha.
Aliongeza kuwa, mbali na umuhimu wa WMAs katika utalii, maeneo haya ya uhifadhi yatawasaidia katika ufugaji wa nyuki, kupata kuni ambayo ndiyo nishati inayotumiwa na kutegemewa na wanakijiji pamoja kuhifadhi vyanzo vya maji katika vijiji.
Ili kufanikisha katika ulinzi, uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za wanyamapori katika Jamii basi vijiji havinabudi kujiwekea mpango wa matumizi ya ardhi, kwani maeneo ya WMAs yanatengwa kwenye ardhi ya vijiji kwa kufuata na kuzingatia mpango wa matumizi bora ya Ardhi.

Wataalamu
kutoa halmashauri za wilaya ya Manyoni na Itigi walizungumzia ukataji
ovyo wa misitu na upasuaji wa mbao ambao haufuati Sheria na kanuni za
misitu. Vitendo hivi vimepelekea uharibi mkubwa wa mazingira katika
wilaya yao ya Manyoni.
Mtaalamu wa misitu alisisitiza kufuata Sheria na taratibu za uvunaji wa misitu. Aidha, Afisa wanyamapori wa Wilaya alizungumzia suala ya wanyama wakali na waharibifu wa mazao, pamoja na taratibu za kufuata endapo wanapatwa na matatizo hayo.
Alieleza na kufafanua viwango vya malipo kwa wananchi wanaopatwa na madhara ya wanyamapaori na kuwataka wasifanye shughuli za kijamii karibu na mipaka ya Pori la Akiba.

No comments