CCM YAWATIMUA WASALITI Wasaliti wa 2015 Watupiwa Virago Huko Arusha,Yumo Bilionea Mkubwa Nchini.

CHAMA cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha
inadaiwa kimewafukuza uanachama baadhi ya vigogo wake akiwamo Mwenyekiti
wa chama hicho Wilaya ya Arusha, Wilfred Soileli.
Wanachama hao wanatuhumiwa kukisaliti
chama hicho kabla na baada ya uchaguzi mkuu wakidaiwa kuwa wafuasi
watiifu kwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.
Wengine waliotimuliwa ni Mjumbe wa
halmashauri kuu ya taifa kutoka jimbo la Arumeru Magharibi Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC ) na mfanyabiashara maarufu wa madini ya
vito, Mathias Manga na Julius Mungure wa Jimbo la Arumeru Mashariki.
Wakati vigogo hao mkoani Arusha
ikielezwa wamevuliwa uanachama wiki iliyopita, Kamati ndogo ya Maadili
ya CCM iliyokutana Dodoma iliwahoji wanachama wake ambao wanadaiwa
kukisaliti chama hicho.
Hao ni Profesa Juma Kapuya, Nazir
Karamagi na Ally Sumaye ambao wote wanadaiwa kukisaliti chama wakati wa
Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Wana CCM hao waliohojiwa na kamati hiyo
iliyoongozwa na Naibu Katibu Mkuu Bara, Rodrick Mpogolo, ambaye gazeti
hili lilipomtafuta kwa simu, haikupokewa.
Taarifa zilizosambaa jijini hapa jana
jioni zilidai uamuzi wa kuwafukuza uanachama viongozi hao ulifanyika
katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Arusha kilichofanyika
Jumamosi chini ya Mwenyekiti wa chama wa mkoa huo, Lekule Laizer.
Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho
walisema kuwa Soileli na Manga walituhumiwa kushirikiana kutoa siri na
mikakati ya chama na kuipeleka kwa viongozi wa Ukawa hasa Lowassa ambaye
alikuwa mgombea wa nafasi ya Rais.
“Hawa walionywa mara nyingi waache tabia
ya kushirikiana na wapinzani hasa Lowassa lakini Manga aliwahi kusema
yuko tayari kuchukuliwa hatua lakini asingeacha urafiki wake na Lowassa
kwani siasa siyo uadui,” alisema mmoja wa wajumbe wa kikao hicho ambaye
hakutata kutwa jina .
No comments