JAJI SEKELA:MAHAKAMA INATEGEMEA USHIRIKIANO MKUBWA KUTOKA KWA WADAU WENGINE ILI KUWEZESHA UKUAJI WA UCHUMI
![]() | |||
|
| Maheshimiwa Majaji wakiwa wanabadilishana mawili matatu kama wanavyoonekana katika picha na mstahiki meya wa Jiji la Arusha Calist Lazaro.Picha na Vero Ignatus Blog. |
| Wakili Magdalena Sylister akisalimiana na Mwandishi wa habari John Muhala katika maadhimisho ya siku ya sheria nchini .Picha na Vero Ignatus Blog. |
|
Waheshimiwa majaji pamoja na mkuu wa mkoa wa Arusha wakiwa katika picha ya pamoja na mahakimu katika siku ya maadhimisho ya sheria nchini katika viwanja vya mahakama kuu kanda ya Arusha picha na Vero Ignatus Blog.
|
![]() | ||
Askari Polisi ,pamoja na na askari wa Jeshi la Magereza wakiwa pamoja katika Mahakama kuu Kanda ya Arusha katika maadhimisho ya siku ya sheria nchini.Picha na Vero Ignatus Blog.
|
| Baadhi ya Mahakimu na Mawakili wa Serikali na wale wa kujitegemea wakiwa katika viwanja vya Mahakama kuu Kanda ya Arusha wakiwa katika maadhimisho ya siku ya sheria nchini.Picha na Vero Ignatus Blog. |
| ||
![]() |
Mhe,Jaji Dk.Modesta Opiyo Jaji wa mahakama kuu Kanda ya Arusha akitoa neno la shukrani kwa wageni mbalimbali waliohudhuria katika siku ya sheria nchini.Picha na Vero Ignatus Blog.![]() |
![]() |
| Kikundi cha Burudani kikifanya yao katika maadhimisho ya siku ya sheria nchini katika viwanja vya Mahakama kuu kanda ya Arusha .Picha na Vero Ignatus Blog. |
Wanafunzi wa chuo kikuu Makumira kitivo cha sheria wakiwa katika picha ya pamoja na waheshimiwa Majaji ,mkuu wa mkoa wa Arusha ,katika siku ya sheria nchini .Picha na Vero Ignatus Blog.
Na Vero Ignatus. Blog
Mahakama
kuu kanda ya Arusha imeungana na na mahakama nyingine kuadhimisha siku ya
sheria nchini ambapo ni siku ya kuanza rasmi shughuli za mahakama,ikiwa na Maudhui yanayosomeka ‘Umuhimu wa utoaji
haki kwa wakati kuwezesha ukuaji wa uchumi.
Akisoma
hotuba Kaimu Jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Arusha Jaji Sekela Cyril Moshi amesema kuwa katika
kuadhimisha siku ya sheria 2017 amesema kuwa neono haki katika sheria hasa
mahakama lina maana ya stahiki ambayo mtu anastahili kuipata kwa mujibu wa
sheria ,taratibu na kanuni zilizowekwa katika upatikanaji wa kitu au jambo
hilo.
Jaji
Sekela amesema kuwa ili kuboresha na kufanikisha malengo ya kutoa haki kwa
wakati ili kusaidia kukuza uchumi ,Mahakama inahitaji kuwezeshwa kwa rasilimali
kama fedha za kutosha na pesa hizi zipatikane kwa wakati,upatikanaji wa
rasilimali utasaidia mahakama kutimiza majukumu yake kwa wakati.
Ametoa rai
kwa watu wote kuwa ,malengo haya ya kumaliza kesi kwa wakati ili kuwezesha
ukuaji wa uchumi hayawezi kufanikishwa na mahakama peke yake,inategemea
ushirikiano mkubwa kutoka kwa wadau wengine wakiwemo wadau,mawakili wa serikali
na wakujitegemea,magereza na taasisi zingine za serikali zikiwemo Takukuru
,hivyo ameiomba jamii ishirikiane na kusaidiana ili kufikia malengo
waliyojiwekea
“Vyombo
vyenye mamlaka ya kutekeleza utoaji haki vitakua ni mahakama ya serikali ya Jamhuri ya muungano wa Mahakama ya Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar,Mamlaka
ya utoaji haki jamhuri ya muungano ipo mikononi mwa mahakama ya Tanzania na
mahakama ya Zanzibar ,na kwahiyo hakuna chombo cha serikali wala cha bunge au
Baraza la wawakilishi la Zanzibar kitakachokuwa na kauli ya mwisho katika
utoaji haki”alisema Jaji Sekela.
Amesema
kuwa ibara ya 107A(2)ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka
misingi ya utoaji haki amabayo mahakama inapaswa kuizingatia katika kutekeleza
majukumu yake ya kikatiba,kutenda haki ya mtu kijamii,au
kiutamaduni,kutochelewesha haki bila sababu ya msingi,kutoa fidia ipasavyo kwa
watu wanaoathirika kutokana na makosa ya watu wengine,na kwa mujibu wa sheria mahususi
iliyotungwa na Bunge.
Aidha
amesema kuwa kutenda haki pasipo kufungwa kupita kiasi na masharti ya kiufundi
yanayoweza kukwamisha haki kutendeka,kukuzana kuendeleza usuluhishi baina ya
wanaohusika katika migogoro,ambapo mahakama inawajibika kutenda haki bila
kuchelewa “Haki iliyocheleweshwa ni sawa na haki iliyokosekana”
Kwa upande
wa hotuba iliyosomwa na mwenyekiti wa chama cha mawakili Tanganyika kanda ya
Kaskazini ,wameiomba jeshi la polisi kuwahudumia wananchi kwa weledi na haki
wazingatie sheria,wasitumie nguvu kupita kiasi,na wakamilishe upelelezi mapema
kabla ya kumkamata mtuhumiwa.
Wamewapongeza
Takukuru kwa utendaji wao kwani wamefanikiwa katika ukamataji wa watuhumiwa
baada ya upelelezi kukamilika,mawakili hao wamewataka Jeshi la magereza
wasichoke kuwahudumia mahabusu kwa huruma haswa ikizingatiwa kwamba hao hawajahukumiwa
bado,huku wakiwataka baraza la Ardhi na nyumba wilaya waboreshe utendaji wao.






No comments