VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA, 80 WATIWA NGUVUNI ARUSHA
Pichani
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo
akionyesha baadhi ya kete za Heroin ambazo zilikamatwa hivi karibuni
kutokana na misako inayoenndelea mkoani hapa. (Picha na Rashid Nchimbi
wa Jeshi la Polisi Arusha)
Na
Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Wiki chache baada ya
Jeshi la Polisi mkoani hapa kukamata gunia 58 za bangi ambazo ziliteketezwa
kwa moto na kuharibu hekari 31 za mimea ya
zao hilo katika maeneo ya Kismiri Juu na Engalaon wilayani Arumeru, Jeshi hilo limeendelea
na misako dhidi ya wauzaji, watumiaji na wasafirishaji wa dawa za kulevya na kufanikiwa kuwakata
watuhumiwa 80 katika misako iliyofanyika kwa muda wa siku 4 tu.
Akitoa taarifa hiyo leo
asubuhi ofisini kwake mbele ya waandishi
wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo
alisema kwamba misako hiyo imefanikisha
kukamata jumla ya kete 167 za madawa ya kulevya aina ya Heroin pia misokoto
3,845 ya Bhangi na mirungi kilogramu 33.
“Katika misako hiyo
ambayo ilifanyika wilaya zote sita za mkoa huu, watuhumiwa 54 walipatikana
kwenye tuhuma za Bhangi, 14 ni tuhuma za Heroin na 12 ni wa tuhuma za mirungi.”
Alisema Kamanda Mkumbo.
“watuhumiwa 40 ni
wauzaji wa madawa hayo huku 13 ni wale ambao walikuwa wanajihusisha kwa namna
moja au nyingine na Bhangi na mmoja alikuwa anasafirisha, watuhumiwa 14 wa
Heroin kosa lao kupatikana huku 12 makosa yao ni kupatikana na mirungi na hivyo
kufanya idadi yao kuwa 80 ambao ni wanaume na wanawake”. Alifafanua Kamanda
Mkumbo.
Kamanda wa Polisi aliwashukuru
wananchi wa mkoa huu kwa ushirikiano wa utoaji wa taarifa za uhalifu na
kuwaomba waendelee kufanya hivyo na kutoa onyo kwa wale wachache wanaojihusisha
na uhalifu wa namna hiyo waache mara moja vinginevyo watakamatwa na kufikishwa
kwenye vyombo vya sheria.
No comments