MKALIMANI 'FEKI' ALIYETAFSIRI VISIVYO MATAMSHI YA MTALII AOMBA RADHI...HII HAPA KAULI YAKE
Awali
mkalimani huyo anayeitwa Simon Sirikwa aliwekwa chini ya ulinzi
kutokana kile kilichokuwakinatafsiriwa kudaiwa kuwa kilikuwa kinapotosha
uhalisia wa maneno yaliyokuwa yakizungumzwa na mtalii aliyekuwa
akisifia kile alichokiona baada ya kutembelea eneo hilo la utalii.
Hata
hivyo katika video mpya aliyoitoa akiwa na mtalii yule yule
aliyeonekana katika video ya kwanza, amesikika akizungumza kwa lugha ya
Kiswahili akiomba radhi kwa kile alichokuwa amezungumza kwenye video ya
awali.
"Kama mlivyoona video yangu niliyopitisha mimi ni tour guide kwa
zaidi ya miaka kumi sasa, siwezi kuichafua hii nchi hata kidogo, hata
aliyetoa hiyo video kwenye Facebook, kwenda kwenye Whatsapp na
kuisambaza kwenye makundi ya kijamii atakuwa amekosea," amesema Sirikwa.
"Lakini ilikuwa ni comedy, ilikuwa ni utani, na najua kuna watu wamekwazika, ila naomba samahani kwa waliokwazika, ila kwa mafansi wangu,
wafuasi wangu endeleeni kupata burudani, ila mfahamu sijafanya hichi
kitu kwa serious wala sikuwa na makusudio yoyote mabaya, asanteni."
Baadhi
ya watu wanaomfahamu Sirikwa walipohojiwa na BBC wamemuelezea alivyo
mtu wa utani na kwamba anajulikana kwa jina la utani kama Mpondam
Haijabainika iwapo Sirikwa aliachiliwa huru bila masharti au aliachiliwa huru kwa dhamana.
Mwanamke
mtalii kwenye video hiyo ya pili anasikika akisema: "Hamjambo tena,
Sehemu ya pili ya video yetu. Tunacheza tu. Simon alikuwa anafanya
ucheshi tu na tulikuwa tunafanya utani tu kidogo kwenye Facebook.
Ijumaa,
kamanda wa polisi wa kanda hiyo Jaffari Mohammed aliambia BBC kwamba
mwelekezi huyo alikuwa "amempotosha" mtalii huyo na kwamba polisi
walikuwa wakifanya uchunguzi kubaini iwapo alisambaza video hiyo
mitandao ya kijamii kinyume na sheria za uhalifu wa kimitandao.
Sheria
hiyo inatoa faini ya kuanzia $1,300 (£1,000) na kifungo cha kuanzia
miezi mitatu jela kwa anayepatikana na kosa la kuchapisha habari za
uongo, za kuhadaa au za kupotosha kwa kutumia kompyuta.
Sheria hiyo ilianza kutekelezwa mwaka 2015.
Mwelekezi huyo alikamatwa kwa azigo la Waziri wa Utalii Jumanne Maghembe.
Mwandishi
wa BBC mjini Dar es Salaam anasema kuwa huenda waziri alihisi kuwa
mkalimani huyo alikuwa akimsuta mtalii au alikuwa akimuiga Rais John
Magufuli.
Kwenye video hiyo asili, mtalii anasema:
"Hi.
Ziara yangu nchini Tanzania imekuwa nzuri. watu ni wazui na wenye
urafiki. Salamu kwa kawaida ni Jambo, nina furaha kuwa hapa, Ardhi ni
nzuri."
Mkalimani anatafsiri hivi:
"Anasema
watanzania mnalia sana njaa, kila siku mnalia nja wakati mna maua
nyumbani, si mchemshe maua mnywe, anasema si vizuri kulia njaa."
Mtalii
"Aina nyingi ya wanyama na watu unaona ni wazuri, kinyume na sehemu zingine. Ni nzuri."
Mkalimani
"Anasema mnamuomba rais wenu awapikie chakula, kwani rais wenu ni mpishi, angahikeni mfanye kazi,chemsheni hata nguo mnywe."
Mtalii
"Ni kitu mabacho utakikumbuka katika maisha yako yote. Ni nzuri na ni ya kupendeza."
Mkalimani
"Anasema mhangaikeni pembezoni za nchi, muache rais hawezi kutoka Ikulu akuje kuwapikia chakula, hivyo mjipikie wenyewe."
Via>>BBC
No comments