UVCCM Taifa wafikiria kuibadilisha Vijana Jazz Band kuwa chuo cha Muziki
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka kwa nyakati
tofauti 15 Februari amekutana na kufanya mazungumzo na wasanii wa
muziki nguli hapa nchini akiwemo Msanii Banana Zoro na msanii
mwanadada Stara Thomas waliomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya
UVCCM, Jijini Dare es Salaam.
Katika mazungumzo yake na wasanii hao nguli na wenye mafanikio
makubwa nchini katika medani ya mziki Kaimu Katibu Mkuu alipokea
Ushauri na namna bora zaidi ya kuboresha bendi ya UVCCM VIJANA JAZZ
BAND wana “Saga rumba” ambayo hufanya maonesho yake kila siku ya
Jumapili eneo la Vijana Social Kinondoni.
Hata hivyo, katika mazungumzo hayo, wote kwa pamoja wameahidi
ushirikiano mkubwa katika maboresho makubwa na stahiki kwa bendi ili
sasa ijiendeshe kitaalam.
“Vijana jazz ni bendi iliyojijengea heshima miaka mingi hivyo ni tuna
kila sababu ya kuimarisha ili iweze kujitangaza na kufikia mafanikio
kulingana na mahitajio ya muda tuliona ” alisema Banana.
Kwa upande wake Stara Thomas katika maongezi yake na Kaimu katibu
mkuu alisema “Hii ni bendi inayopaswa sasa kuwa chuo cha muziki kwa
vijana waje wajifunze mziki na kusambaa kwingineko”
Katibu mkuu Ameahidi kufanyia kazi ushauri uliotolewa kwake na
wanamuziki hao kwa ukizingatia kauli mbiu ya CCM Mpya Tanzania Mpya
sambamba na kuongeza soko la ajira kwa vijana kupitia mziki wa dance.
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka akiwa katika mazungumzo hayo
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka akifanya mazungumzo na msanii BananaZorro
No comments