TEA YAINGIA MKATABA WA MAKUBALIANO YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA ELIMU NA KAMPUNI YA SUNSHINE
MAMLAKA ya Elimu Tanzania (TEA) imesaini mkataba wa makubaliano ya utekelezaji wa miradi mbalimbali na Kampuni ya SunShine Group kutoka China kwa miaka mitano kuanzia sasa.
Akizungumza
na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kusaini mkataba huo wa
makubaliano, Kaimu Mkurugenzi wa TEA, Graceana Shirima alisema
makubaliano hayo yataifanya TEA kuwa mratibu wa miradi ya kuboresha
elimu hapa nchini huku Sunshine ikifadhili na kutekeleza miradi hiyo.
Kwa
mujibu wa Shirima miradi hiyo itatekelezwa katika mikoa ya Dar es
Salaam, Mwanza, Dodoma, Mbeya, Mara na Mtwara ambapo miradi ya ujenzi wa
miundombinu ya shule na vifaa itatekelezwa na kampuni hiyo huku
akibainisha kwamba mikoa hiyo ndiyo yenye miradi mikubwa ya kampuni ya
Sunshine.
“Miradi
ya kwanza kutekelezwa kupitia makubaliano haya ni ujenzi wa maabara
mbili za sayansi katika shule za sekondari Matundasi iliyopo Jijini
Mbeya na miundombinu ya maji kwenye sekondari ya Bunda mkoani Mara
ambapo Zaidi ya sh. Milioni 210 zitatumika,” alisema Shirima.
Akiishukuru
TEA, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sunshine Goup, Tony Sun alisema kampuni
yake inaona fahari kusaidia sekta ya elimu Tanzania huku akiahidi
kuendelea kuwekeza katika sekta hiyo muhimu kwa maendeleo ya taifa.
Alisema
kampuni yake imeingia Tanzania mwaka 2012 na tayari imetumia zaidi ya
Dola 500,000 za Marekani katika elimu kwa miaka mitano ya uwepo wao hapa
Tanzania.
“Tumedhamiria
kuboresha elimu ya Tanzania kwa kuhakikisha mazingira ya upatikanaji wa
elimu yanakuwa rafiki na yenye kuvutia. Tunaamini TEA watatusaidia
kuzifikia shule zenye uhitaji zaidi ili watoto wetu wapate elimu bora
kwa ajili ya kujenga taifa imara,” alisema Sun.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Graceana Shirima
akifafanua jambo wakati wa hafla ya kutiliana saini mkataba na
Mkurugenzi Mtendaji wa Sunshine Group Ltd, Tony Sun, ya makubaliano ya
miaka mitano ya kushirikiana katika kuratibu na kufadhili miradi ya
elimu nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Sunshine Group Ltd, Tony Sun, ya makubaliano ya miaka mitano ya kushirikiana katika kuratibu na kufadhili miradi ya elimu nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Sunshine Group Ltd, Tony Sun, ya makubaliano ya miaka mitano ya kushirikiana katika kuratibu na kufadhili miradi ya elimu nchini.
Mkutano ukiendelea.
Kaimu Mkurugenzi wa Mipango, Dk. Erasmus Kipesha akisaini mkataba wa makubaliano hayo.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Graceana Shirima
(kushoto), akisaini mkataba na Mkurugenzi Mtendaji wa Sunshine Group
Ltd, Tony Sun, wa makubaliano ya miaka mitano ya kushirikiana katika
kuratibu na kufadhili miradi ya elimu nchini.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Graceana Shirima
(kushoto), akibadilishana mkataba na Mkurugenzi Mtendaji wa Sunshine
Group Ltd, Tony Sun, ya makubaliano ya miaka mitano ya kushirikiana
katika kuratibu na kufadhili miradi ya elimu nchini.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Graceana Shirima
(kushoto), akibadilishana mkataba na Mkurugenzi Mtendaji wa Sunshine
Group Ltd, Tony Sun, ya makubaliano ya miaka mitano ya kushirikiana
katika kuratibu na kufadhili miradi ya elimu nchini. Kushoto
anayeshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi wa Mipanga, Dk. Erasmus Kipesha na
Mwakili Mkazi wa Sunshin Group, Harison May.
No comments