Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli,
amemteua Bw. Omary Rashid Nundu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya
Simu Tanzania (TTCL).
Taarifa
iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa
uteuzi wa Bw. Omary Rashid Nundu umeanza tarehe 24 Februari, 2017.
Bw. Omary Rashid Nundu anachukua nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Prof. Tolly Salvatory Augustine Mbwete.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemuapisha Thobias Emir Andengenye kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Kamishna Jenerali Thobias Emir Andengenye anachukua nafasi ya Kamishna Jenerali Pius M. Nyambacha ambaye amestaafu.
Pia, Mhe. Rais Magufuli amewaapisha Mabalozi wanne walioteuliwa kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali kama ifuatavyo;
Mhe.
Dkt. Pindi Hazara Chana ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania Nairobi,
Kenya ambako anachukua nafasi ya Mhe. John Haule ambaye amestaafu.
Mhe. Silima Kombo Haji ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania Khartoum, Sudan ambako anakwenda kufungua Ubalozi.
Mhe.
Abdallah Abas Kilima ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania Muscat, Oman
ambako anachukua nafasi ya Mhe. Ali Ahamed Saleh ambaye amestaafu.
Mhe. Matilda Swila Masuka ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania Seoul, Korea Kusini ambako anakwenda kufungua Ubalozi mpya
Aidha
Mhe. Rais Magufuli ameshuhudia Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto
na Uokoaji na Mabalozi wote wanne wakila kiapo cha uadilifu kwa viongozi
wa ummakilichoongozwa na Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Mstaafu Harold
Nsekela.
Hafla
ya kuapishwa kwa viongozi hao imehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia
Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba na viongozi wa vyombo
vya ulinzi na usalama.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha
Balozi Pindi Chana kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya, tukio
lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha
Balozi Silima Kombo Haji kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sudani, Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha
Balozi Abdallah Kilima kuwa Balozi wa Tanzania nchini Oman, Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha
Balozi Matilda Masuka kuwa Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini,
Ikulu jijini Dar es Salaam.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akila kiapo
cha Ahadi ya Uadilifu pamoja na Mabalozi Pindi Chana, Balozi Silima
Kombo Haji, Abdallah Kilima pamoja na Balozi Matilda Masuka mara baada
ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU
No comments