Serikali yaahidi kuendeleza vita ya kuzuia vitendo vya ukeketaji kwa wanawake
Serikali ya Tanzania imesema
itaendeleza vita kupinga vitendo vya ukeketaji ambavyo wamekuwa
wakifanyiwa wanawake na wasichana katika maeneo mbalimbali nchini kwani
hicho ni kinyume na sheria ya Tanzania na ni ukiukwaji wa haki za
wanawake.
Hayo yamesemwa na Naibu Spika wa Bunge, Dk. Ackson Tulia katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na Balozi wa Italia nchini kwa lengo la kubadilishana uelewa kuhusu ukeketaji na jinsi umevyoathiri jamii ya Tanzania.
Naibu Spika wa Bunge, Dk. Ackson Tulia.
“Serikali inafanya jitihada
mbalimbali kumaliza vitendo hivi vya kikatili ambavyo wanafanyiwa
wanawake ikiwepo kutoa elimu kwa kutumia vyombo vya habari …
niwahakikishie Bunge la Tanzania na Serikali kwa ujumla itaendelea
kushirikiana na wadau kupambana kumaliza vitendo vya ukeketaji kwa
wanawake na wasichana,” alisema Dk. Tulia.
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini, Roeland Van De Geer.
Nae Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini,
Roeland Van De Geer alisema EU imekuwa na mipango mbalimbali ambayo
imekuwa ikifanya kwa ajili ya kusaidia nchi ambazo zimebainika kuwepo
kwa vitendo vya ukeketeaji kumaliza vitendo hivyo na itandelea
kushirikiana na Serikali kuhakikisha vitendo hivyo vinamalizika.
“EU ilitenga pesa kwa ajili ya kusaidia wanawake na wasichana na moja na mipango ya pesa hiyo ni kumaliza vitendo vya ukeketaji, EU inaamini kuwa wanawake wanahusika sana katika shughuli za maendeleo na ni muhimu kwao kulindwa na jamii nzima ili wawe salama,” alisema Van De Geer.
Balozi wa Italia nchini Tanzania, Roberto Mengoni.
Nae Balozi wa Italia nchini, Roberto
Mengoni alisema Serikali ya nchi yake inapinga vitendo hivyo na tayari
inashirikiana na Serikali za nchi za Afrika zilizo na vitendo vya
ukeketaji na Tanzania ikiwa ni mojawapo, hivyo wataunga mkono juhudi za
Serikali kuelimisha jamii iachane na vitendo hivyo.
Takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania ni moja ya nchi 29 za Afrika ambazo wanawake wa nchi hizo wanafanyiwa ukeketeaji ambapo asilimia 14.6 ya wanawake nchini wanakadiriwa kufanya vitendo hivyo na mkoa wa Manyara ukiongoza kwa asilimia 58 kwa wanawake wanaoishi katika mkoa huo kufanyiwa vitendo vya ukeketaji.

Hayo yamesemwa na Naibu Spika wa Bunge, Dk. Ackson Tulia katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na Balozi wa Italia nchini kwa lengo la kubadilishana uelewa kuhusu ukeketaji na jinsi umevyoathiri jamii ya Tanzania.
Dk. Tulia alisema Serikali inatambua
kuwepo kwa sehemu ambazo zimekuwa zikifanya vitendo hivyo na itaendelea
juhudi zake za kuzuia vitendo hivyo na kumaliza kabisa na itandelea
kushirikiana na mataifa na mashirika mbalimbali ambayo yanaunga mkono
mpango wa Serikali wa kumaliza vitendo hivyo.

No comments