CHAMA CHA WAALIMU MKOANI ARUSHA WAMUUNGA MKONO WAZIRI MKUU

Image result for VIROBA 
Na.Vero Ignatus ,Arusha.
 
Chama cha walimu mkoa wa Arusha,imeazimia kuungana na Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa kupiga vita utumiaji na uzaji wa viroba

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapo, Mwenyekiti wa Chama cha walimu jiji la Arusha,Joyce  Msaki amesema walimu mkoa wa Arusha wameunga mkono jitihada za waziri mkuu juu  kupambana na utumiaji wa viroba  kwakua shule pia zimeathiriwa na  utumiaji wa pombe hizo

Wiki iliyopita Waziri Mkuu Kassim Majaaliwa,akiwa kwenye ziara mkoani Manyara alitoa tamko la kuzuia matumizi pamoja na uuzwaji wa pombe aina ya viroba na kusema mpaka ifikapo tarehe 1 machi vinywaji hivyo viwe haviuzwi tena

Hata hivyo ,alisema utumiaji wa pombe hizo mashuleni umesababisha nidhamu kushuka kwa wanafunzi ikiwa baadhi ya walimu kuambuliwa kupigwa na wanafunzi ambao wametumia pombe hizo


Pia alisema,kutokana na urahisi wa pombe hizo ilikuwa ngumu kwao kudhibiti hasa wanafunzi kuwa na mtindo kuchanganya kwenye maji na kwenda nazo mashuleni

"Mtindo uliokuwepo walikuwa wanavikata wanachanganya maji,hivyo inakuwa ngumu kutambua utakachogundua baadae ni tabia yake baada ya kutumia,"alisema Jocye

"Walimu mkoa wa Arusha tunampongeza Waziri Mkuu kwa vita aliyoanzisha na tunahaidi kupambana kwenye vita hii ili wanafunzi waweze kufanya vizuri kwenye masomo yao,"alisema Jocye


Pia alisema ipo sababu ya serikali kuzingatia sheria ya utengenezaji wa pombe nchini hasa kwakusisitiza upakiaji wa pombe hizo uwe wa ujazo mkubwa na si kwenye vifungashi vya viroba

Mwanafunzi unakuta anapewa 1000 hadi 2000 ya nauli,kiroba kinauzwa bei 500 hadi 600, kwa bei hii ni raisi kununua lakini mfano konyagi ndogo 3500 na kubwa 7000 kwa mwanafunzi kununua ni ngumu,bora ziuzwe ghali iliwashindwe kununua,"alisema Jocye

Wakati huohuo,Katibu wa Walimu jiji la Arusha,Nuruel Kavishe alisema agizo la Waziri Mkuu litarahisisha walimu kufundisha mashuleni hasa wanafunzi kuwa na uwezo mkubwa wa kuelewa kuliko awali ilivyokuwa

"Tunaushaidi mkubwa kuwa kweli wanafunzi wanatumia viroba hasa wanafunzi wa shule za sekondari,sisi tutamsaidia Waziri kupambana na vita hii

Hata hivyo,alisema kama walimu baada ya tarehe 1 machi kufika kama viroba vitaendelea kuuzwa ,watatoa taarifa kwa Waziri mkuu ikiwa ni pamoja na kumpelekea majina ya wauzaji wa pombe hizo

Mwakilishi wa walimu vijana mkoa wa Arusha  Denis Lubida alisema licha ya pombe hizo kukatazwa zitasaidia kuwepo kwa dhana ya uwajibikaji kwanzia mwanafunzi,mzazi pamoja na walimu

Akiendelea kusema hivyo alisema pombe hizo hazikumuathiri mwanafunzi peke hata waalimu pia waliathiriwa na pombe hizo


No comments