Waziri Ummy Mwalimu afungua mkutano wa Dunia wa masuala ya udhibiti wa kifua kikuu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummuy
Mwalimu amefungua rasmi mkutano wa Dunia wa masuala ya kudhibiti Kifua
Kikuu ulioshirikisha wadau mbalimbali nchini.
Waziri
wa Afya ,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummuy Mwalimu
akihutubia wadau (hawapo pichani) wa kifua kikuu toka nchi mbalimbali
walioshiriki Mkutano wa Dunia wa 12 wa masuala ya Kudhibiti Kifua kikuu
unaofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency jijini hapa.
Mganga
Mkuu wa Serikali Prof. Mohammad Bakari Kambi akiwasilisha mada mada
kwenye mkutano huo ambao unafanyika kwa siku tatu na umewashirikisha
Serikali,Sekta binafsi,Mashirika Binafsi na wadau mbalimbali wa afya.
Waziri Ummy Mwalimu akifuatalia Mada iliyokuwa ikiwasilishwa,kulia ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammad kambi
Washiriki mbalimbali wa mkutano huo wakifuatilia mada zinazowasilishwa kwenye mkutano huo
Waziri ummy Mwalimu akionesha kitabu cha mapambano dhidi ya kifua kikuu chenye mikakati mbalimbali ya kudhibiti ugonjwa huo.
Picha
ya pamoja ya washiriki wa Mkutano wa Dunia wa 12 wa masuala ya
Kudhibiti kifua Kikuu Duniani.Nchi zilizohudhuria mkutano huo Afrika
(Tanzania, Ethiopia,Kenya, Malawi, Namibia, Uganda ,Zambia na Afrika
kusini) nchi za Asia ni (India,Pakistan,Bangladesh) Picha zote na
Rayson Mwaisemba-Wizara ya Afya)
No comments