ASKOFU GWAJIMA ALIPOZUNGUMZA NA WANAHABARI JUU YA KUTAJWA KWAKE SAKATA LA DAWA ZA KULEVYA
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Askofu
wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josepahat Gwajima amesema kuwa ameokoka
na anamtumikia mungu hivyo kutajwa katika orodha ya wanaojihusisha na
dawa za kulevya iliyotangazwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ni jambo
ovu.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Askofu Gwajima
amesema kuwa Mkoa wa Dar es Salaam anafanya kazi vizuri lakini suala la
kiutawala hawezi na kumuomba Rais Dk. John Pombe Magufuli ambadilishie
kazi.
Amesema
yeye alikuwa Mpwapwa katika kazi zake aliposikia kutajwa kwa jina lake
na kumlazimu arudi na kuwasili pale alipoitwa bila kusubiri siku
iliyopangwa ya kukutana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Askofu
Gwajima amesema kuwa kuhusu mali anazomiliki ni kutokana na kazi
anazofanya ikiwa kuwa na kampuni mbalimbali pamoja na kufundisha masuala
ya farsasafa nje nchi na kulipwa dola za kimarekani 1000 kwa saa.
Aidha
amesema kuwa kulindwa kwake ni kutokana na kuwa na usalama wake hata
papa ana gari ambayo haipiti risasi wakati ni mtakatifu.
Askofu Gwajima amesema Makonda anachuki na wivu dhidi yake ndio maana anamhusisha na jambo ovu ambalo linamchafu mbele ya mungu.
Amesema kuwa yuko radhi kukaa ndani miaka 40 kutokana na kupigania suala la uovu ni jambo halitawe za kuvumiliwa.
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,
Josepahat Gwajima akizungumza na waandishi wa habari juu ya kutajwa
kwao kujihusisha na dawa za kulevya leo jijini Dar es Salaam.picha na
Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
Katibu
Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Gwandu Mwangasa akizungumza na
waandishi wa habari juu watavyopambana na katika kupigania Askofu wake
Josephat Gwajima leo jijini Dar es Salaam.
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josepahat Gwajima akitoka katika mkutano na kuelekea kituo Kikuu cha polisi leo jijini Dar es Salaam.
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josepahat Gwajima akiagana na waumini wa kanisa hilo leo jijini Dar es Salaam.
No comments