ANG'ATWA ULIMI NA MWANAMKE KILABUNI



TAARIFA zilizotufikia zinasema kuwa mwanaume mmoja huko Inyala Mbeya Vijijini kusini mwa Tanzania, amelazwa katika kituo cha Afya cha Inyala baada ya kung'atwa ulimi na mwanamke aliyekuwa amekutana naye katika kilabu cha pombe za kienyeji na kuanza kucheza naye muziki na kumnyonya ulimi wake.

Tukio hilo limetokea juzi kijijini hapo ambapo imeelezwa kuwa kijana huyo alikuwa mgeni kwa wenyeji wa maeneo hayo.

Mwenyekiti wa Kijiji hivcho ndugu Agata Njima, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

No comments