AJALI YA MAGARI MAWILI ,PIKIPIKI YAUA WATU SABA MOSHI,YUMO MWANDISHI WA HABARI NA MWENYEKITI WA CCM
WATU saba wamepoteaza maisha papo hapo katika tukio la ajali ya
barabarani iliyotokea leo jioni Jumapili February 5,2017 katika eneo la
Mwika mpakani mwa Wilaya ya Rombo na Moshi Vijijini Mkoani Kilimanjaro.
Waliopoteza maisha ni pamoja na Mwandishi wa gazeti la Habarileo ambaye
pia alikuwa Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Hai, Anorld Swai.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,SACP,Wilbroad Mutafungwa
alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa ajali ilitokea
majira ya saa 11 jioni ikihusisha magari mawili na pikipiki maarufu kama
Bodaboda.
“Ajali imetokea majira ya saa 11 jioni ambapo watu saba wamepoteza
maisha wanne ni kutoka katika Toyota Surf T606 AQZ, mmoja katika
bodaboda MC 101 ANC huku wengine wakiwa ni kwenye Fuso T343 BNL,”alisema
Kamanda Mutafungwa.
Alisema ajali hiyo ilitokea katika eneo la Mwika katika Kijiji cha
Mawanjeni katika mpaka wa Wilaya ya Rombo na Wilaya ya Moshi Vijijini na
kusema kuwa chanzo cha ajali hiyo inaweza kuwa ni kuharibika kwa mfumo
wa Breki wa Fuso iliyokuwa imebena ndizi ikitokea Rombo kwenda Jijini
Dar es Salaam.
Mbali na Swai wenginw waliopoteza maisha na kutambulika ni Mjumbe wa NEC
ya CCM na Katibu wa CWT kutoka Same Ally Mbaga, Mwenyekiti wa UWT
Anastazia Malamsha, Edwin Msele, Mwanafunzi wa mwaka wanne Chuo cha
KCMC.
Majeruhi wa ajali hiyo ni Jackson Kimambo - Mwandishi gazeti la Nipashe -
amekimbizwa Hospitali ya KCMC kwa Matibabu pamoja na Mwendesha
Bodaboda.
Anord Swai enzi za uhai wake
Ujumbe Anord Swai aliotuma kwenye group la Whatsapp kabla ya kifo chake leo alasiri saa 9.20
Marehemu Anord Swai enzi za uhai wake
Marehemu Anord Swai enzi za uhai wake
Picha za ajali ya mkoani Kilimanjaro



No comments