Serikali kuwa chukulia hatu wanaobadili maeneo ya makazi ya watu na kufanya kuwa ya kibiashara
Serikali
imesema itawachukulia hatua kali za kisheria wananchi waliobadili
matumizi ya Ardhi ya makazi na kuyageuza kuwa maeneo ya biashara na
kuisababishia Serikali kukosa mapato ya kodi ya Ardhi.
Hayo
yamebainishwa jijini Dar es salaam na Kaimu Mkuu wa Kitengo Cha Kodi
toka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Bi.Rehema Kilonzi
wakati  akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu mapato
yaliyokusanywa kutokana na kodi ya pango la ardhi kwa mwaka fedha
2015/2016.
Amesema
kuwa baadhi ya wananchi katika maeneo mbalimbali nchini wameyageuza
maeneo yaliyopangwa kwa ajili ya makazi ya watu kuwa nyumba za kulala
wageni,hosteli, maeneo ya biashara kinyume cha Sheria ya Ardhi Namba 4
ya mwaka 1999 chini ya fungu la 33.
â€Å“Rai
yetu kwa wananchi waliopata fursa ya kumiliki maeneo yaliyopangwa na
kumilikishwa kisheria,tunawaomba walipe kodi ya Pango la ardhi kwa
wakati kuepuka usumbufu wa kufikishwa Mahakamani .â€alisisitizaÂ
Kilonzi.
Amesema
katika kipindi cha mwaka wa 2015/2016 Serikali imefanikiwa kukusanya
kiasi cha Bilioni 60 kutokana na kodi ya Pango la Ardhi ambazo ni sawa
na asilimia 85 ya lengo lililowekwa la kukusanya shilingi bilioni 70.
AmesemaÂ
mkakati wa wizara  hiyo ni kuhakikisha kuwa inafikia lengo la
kukusanya Kodi  hiyo na kuongeza kuwa hiyo imesambaza maafisa wake
katika Ofisi zote za Kanda ili kuhakikisha kuwa Halmashauri na Manispaa
zinasambaza hati za madai ya Kodi ya pango la Ardhi na kuwafikia wadaiwa
wote kwa wakati muafaka.
Baadhi
ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Wizara ya Ardhi Nyumba
na Maendeleo ya Makazi kuhusu mkakati wa Serikali kuwachukulia hatua
 za kisheria wananchi waliobadili matumizi ya Ardhi ya makazi na
kuyageuza kuwa maeneo ya biashara na kuisababishia Serikali kukosa
mapato yanayostahili.
Amesema
wizara hiyo inaendelea na mkakati wa kufungua mashauri ili kupata
kibali cha mahakama cha kukamata mali za wadaiwa sugu na  kuwapokonya
hati milki katika maeneo mbalimbali nchini.
Akizungumzia
hatua hiyo amesema kuwa katika  jiji la Dar es salaam mashauri
yataanza kusikilizwa katika Baraza ya Nyumba na Ardhi La Wilaya ya
Kinondoni kuanzia mwezi Mei 2016, Â kisha zoezi hilo litaendelea kwa
Mikoa na Wilaya zote Jijini hilo.
Akitoa
ufafanuzi kuhusu Kodi ya Ardhi inayotozwa na wizara hiyo amesema kuwa
 inatozwa kwa kuzingatia Sheria ya Ardhi Namba 4 ya mwaka 1999 chini ya
fungu la 33.
Amesema
kuwa katika kipindi cha mwezi mmoja na nusu ( kuanzia Februari 2016)
Wizara imewafikia wamiliki wa Ardhi 679 katika Maeneo ya Sinza na
Kijitonyama Jijini Dar es salaam na kufanya uthamini wa maendelezo kwa
kwa wale waliokiuka masharti ya matumizi yaliyopangwa ambapo ilibainika
kuwa kuna ukiukwaji wa masharti ya Uendelezaji kwa kubadili matumizi
yaliyoainishwa katika milki zao.
Aidha,
amesema kutokana na uthamini uliofanyika mwezi Februari Serikali
inatarajia kukusanya jumla ya milioni mia nane kama faini kutokana na
ubadilishaji wa matumizi ya maeneo usiozingatia Sheria za Ardhi katika
maeneo ya Sinza na Kijitonyama.
Imeandaliwa na Frank Mvungi-Maelezo
Kaimu
Mkuu wa Kitengo Cha Kodi toka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Bi.Rehema Kilonzi   akitoa taarifa kwa waandishi wa habari
kuhusu mapato yaliyokusanywa kutokana na kodi ya pango la ardhi kwa
mwaka fedha 2015/2016 ambapo Serikali imekusanya zaidi ya Bilioni 60
kati ya bilioni 70 zilizopangwa.kulia kwake ni mwanasheria toka Wizara
hiyo Bw.Seif Hiza na mwisho ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini wa Wizara hiyo Bi Mboza Lwandiko.
No comments