Waandamana kupinga ongezeko la bei ya petroli Mexico
Mamia ya
waandamanaji kutoka katika majimbo kumi na mbili nchini Mexico
wameendelea na maandamano na kufunga barabara wakilalamikia ongezeko la
asilimia ishirini ya bei ya mafuta ya Petrol.
Zaidi ya watu mia tano wamekamatwa na maduka mengi yamevamiwa.
Wanasiasa wa upinzani wamewaasa wananchi kuwa na subira na kwamba waandamanaji wasijihusishe katika masuala ya uvamizi na vitendo vya uharibifu
No comments